sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Matukio tuliyoyapa uzito wiki hii duniani
Rais wa DRC Felix Tshisekedi
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Haraka
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May atangaza kujiuzulu
Afrika

UN: Watu milioni 68.5 duniani kote waliyahama makazi yao mwaka 2017

media Lusenda, Kusini mwa Kivu, DR Congo: wakimbizi wapya wkiwasili katika kambi ya Lusenda ambako wamepokelewa na Tume ya Taifa ya Wakimbizi (CNR) na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR). Photo MONUSCO/Abel Kavanagh

Idadi ya wakimbizi na watu waliokimbia makazi yao kufuatia migogoro duniani imefikia mwaka 2017 rekodi mpya. kwa mwaka wa tano mfululizo, hadi milioni 68.5, karibu nusu yao ikiwa ni watoto, Umoja wa mataifa umesema Jumanne wiki hii.

Mgogoro nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, vita nchini Sudan Kusini na mamia ya maelfu ya watu kutoka jamii ya Rohingya kukimbilia Bangladesh kutoka Burma vimesababisha idadi ya watu waliyotoroka makazi yao kuongezeka na kupelekea rekodi mpya mwaka 2017, kulingana na ripoti ya kila mwaka ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR).

Kwa mujibu wa takwimu, idadi ya waimbizi iliyoorodheshwa mwaka 2017 ( "milioni 3.1) inazidi na mbali ile ya mwaka 2016 ( '300,000) na kuelezwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa kwa idadi ya wakimbizi, huku idadi ya wakimbizi wa ndani ikishuka kidogo.

Kwa jumla, hii inamaanisha kwamba mmoja kati ya watu 110 ni mkimbizi duniani kote.

Kwa mujibu wa UNHCR, "wakimbizi waliotoroka nchi zao kwa kuepuka migogoro na mateso ni milioni 25.4 kwa jumla ya watu milioni 68.5 waliohama makaazi yao, sawa na ongezeko la milioni 2.9 zaidiikilinganishwa na mwaka 2016 na pia ongezeko kubwa zaidi lililoorodheshwa na UNHCR kwa mwaka mmoja ".

Wakati huo huo, idadi ya wakimbizi ambao walikuwa bado wanasubiri kupata kibali cha ukimbizi mwishoni mwa mwaka 2017 iliongezeka kwa 300,000 hadi milioni 3.1. Wakimbizi wa ndani katika nchi zao ni milioni 40, takwimu ambayo imepungua kidogo.

Syria bado ni nchi yenye idadi kubwa yawakimbizi, ikifuatiwa na Colombia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Afghanistan.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana