Pata taarifa kuu
DRC-JOSEPH KABILA-SIASA

Wabunge DRC kutunga sheria ya kuwalinda marais waliostaafu

Wabunge nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanatarajiwa kukutana kwa lengo la kutunga sheria ya kuwalinda marais wanaostaafu.

Rais Joseph Kabila amekuwa madarakani kama rais wa DRC, tangu mwaka 2001
Rais Joseph Kabila amekuwa madarakani kama rais wa DRC, tangu mwaka 2001 REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Spika wa bunge Aubin Minaku amesema, rais Kabila ameomba kuwa wabunge wakutane na kujadili na kupitisha sheria hiyo, haraka iwezekanavyo.

Hii ni dalili kuwa huenda rais Kabila ataheshimu Katiba na kutowania tena urais wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwezi Desema, licha ya wasiwasi kuwa huenda akaamua kwuania tena.

Wiki hii, Waziri Mkuu Bruno Tshibala alisema rais Kabila ataheshimu Katiba na hatawania urais kwa muhula wa tatu kinyume na Katiba.

Rais Kabila amekuwa akiongoza nchi hiyo tangu mwaka 2001.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.