Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Hatima ya Bemba kuachiwa au la kujulikana Jumanne hii

media Jean-Pierre Bemba, kiongozi wa zamani wa kivita DRC. REUTERS/Michael Kooren

Siku chache tu zikiwa zimepita tangu majaji katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC wamfutie makosa ya uhalifu wa kivita na dhulma dhidi ya binadamu makamu wa rais wa zamani wa DRC Jean-Pierre Bemba, leo mahakama hiyo itatoa uamuzi ikiwa Bemba ataachiwa huru au la.

Hata hivyo wataalamu wa masuala ya sheria za kimataifa wanasema kunau wezekano mkubwa kiongozi huyo wa zamani wa kivita kuachiwa huru.

Ofisi ya mwendesha mashitaka ya ICC ilishindwa kutoa ushahidi tosha unaomuhusisha Bemba katika uhalifu uliotekelezwa na wapiganaji wake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Jean-Pierre Bemba mwenye umri wa miaka 55 alikataa rufaa mwezi Juni 2016 kwa uamuzi wa ICC kumpata na kosa la kuhusika katika mlolongo wa mauaji na ubakaji, vitendo vilivyofanywa na wanamgambo wake wa kundi la waasi la MLC, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kati ya mwezi Oktoba 2002 na mwezi Machi 2003.

Katika muda wa miezi mitano, wapiganaji 1,500 wa MLC waliua, waliiba na kubaka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambapo walikwenda kumsaidia rais Ange-Félix Patassé dhidi ya jaribio la mapinduzi lililoendeshwa na Jenerali François Bozizé.

Kesi yake iliyofunguliwa mjini Hague mnamo mwezi Novemba 2010, ilikuwa ni ya kwanza ya ICC iliyolenga ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia kama uhalifu wa kivita na kumuhusisha kiongozi mkuu wa jeshi kutokana na uzembe kwa watu waliokua chini ya uongozi wake

Hukumu ya kifungo cha miaka 18 ni hukumu kubwa kabisa kuwahi kutolewa na mahakama hiyo ilianzishwa mwaka 2002 ili kuhukumu uhalifu mbaya unaotekelezwa duniani.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana