Pata taarifa kuu
NIGER-USLAMA

Tisa wauawa katika mashambulizi Kusini-Mashariki mwa Niger

Watu wasiopungua tisa waliuawa katika mfululizo wa mashambulizi ya kujitoa mhanga katika mji mkuu wa jimbo la kusini mashariki mwa Niger, Diffa, karibu na Nigeria, afisa mmoja ameliambia shirika la habari la AFP Jumanne wiki hii. Matukio hayo yalitokea usiku wa kuamkia Jumatatu wiki hii.

Askari wa Niger wakipiga doria kwenye mpaka na Nigeria, karibu na mji wa Diffa, Niger.
Askari wa Niger wakipiga doria kwenye mpaka na Nigeria, karibu na mji wa Diffa, Niger. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Washambuliaji watatu wa kujitoa mhanga walijilipua, kwa sasa watu tisa ndio wamefariki na wengine kadhaa walijeruhiwa," afisa mmoja ambaye hakutaja jina lake ameliambia shirika la habari la AFP. Mji wa Diffa umeendelea kukabiliwa na mashambulizi ya kundi la Boko Haram .

Vyanzo vingine vya habari vinasema kuwa kando ya mauaji hayo, watu wengini wengi walitekwa nyara wakati wa mashambulizi hayo. Wanawake na watoto zaidi ya arobaini ni miongoni mwa watu hao ewaliotekwa nyara kwa mujibu wa gazeti la AFRICA No 1.

"Mashambulizi hayo yalilenga kijiji cha Ngalewa, km chache kutoka mji wa Kabaléwa, kaskazini mwa mji wa Diffa, mji ambao siku ya Jumatano wiki iliyopita ulikumbwa na mashambulizi ya kujitoa mhanga yaliyoendeshwa na wanawake wawili dhidi kambi ya wakimbizina kusababisha vifo vya watu wawili na wengine 11 kujeruhiwa, Meya wa mji huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.