Pata taarifa kuu
SENEGAL-HAKI

Senegal: Kesi ya Khalifa Sall yaahirishwa tarehe 9 Julai

Nchini Senegal, Khalifa Sall amesikilizwa mbele ya majaji wa Mahakama ya Rufaa Jumanne asubuhi wiki hii. Mahakama imeamua kuahirisha kesi hiyo hadi Julai 9.

Kesi ya Khalifa Sall katika Mahakama ya Rufaa imeahirishwa hadi Julai 9.
Kesi ya Khalifa Sall katika Mahakama ya Rufaa imeahirishwa hadi Julai 9. RFI/GUillaume Thibault
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wengi wa meya huyo wa Dakar wawalionekana ndani na nje ya mahakama.

Khalifa Sall, ambaye anazuiliwa jela tangu mwezi Machi 2017, alipatikana na hatia ya udanganyifu na sio ubadhirifu wa fedha za umma.

Serikali, ambayo ilikua ikidai kutendewa haki kwa kulipwa fedha zote zilizoibwa na fidia pia, ilikataa rufaa dhidi ya hukumu ya miaka mitano aliyopewa Khalifa Sall. Ofisi ya mashitaka inaona kwamba adhabu hiyo haitoshi. Wanasheria wa Khalifa Sall wanasema mteja wao hana hatia.

Kwa upande wa wanasheria wa serikali ya Senegal, wanasema kesi hii katika Mahakama ya Rufaa ni muhimu. Kwa sababu serikali ilifanyiwa unyonge katika mahakama ya mwanzo na imeomba kulipwa fedha zilizoibwa.

Ikiwa imesalia miezi minne tu kabla ya uchaguzi wa urais, ambapo Khalifa Sall anaweza kuwania katika uchaguzi huo, bado kesi yake inaendelea kuibua sintofahamu kwa wanasiasa nchini Senegal.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.