Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Waziri Mkuu wa Madagascar ajiuzulu

media Waziri Mkuu wa Madagascar, Olivier Mahafaly Solonandrasana, atangaza kujiuzulu ili kuiondoa nchi yake katika mgogoro wa kisiasa. © RIJASOLO - AFP

Waziri Mkuu wa Madagascar Olivier Mahafaly Solonandrasana ametangaza kujiuzulu wakati ambapo nchi hiyo ikiendelea kukabiliwa na mgogoro wa kisiasa. Kuanzia sasa serikali ya umoja wa kitaifa inatarajiwa kuundwa.

Olivier Mahafaly Solonandrasana amechukua hatua hiyo kufuatia ombi la Mahakama Kuu ya Katiba katika hali ya kumpata waziri mkuu mpya kutoka makubaliano baina ya wanasiasa.

Hivi karibuni Mahakama Kuu ya Katiba ilitoa agizo kwa rais wa Madagascar kufuta serikali yake na kumteua waziri mkuu mpya anayeungwa mkono na vyama vyote vya kisiasa nchini humo.

Hii ni hatua ya kwanza kueekea uteuzi wa waziri mkuu mpya kutoka makubaliano katika hali ya kuondokana na mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Madagascar.

Mnamo mwezi Aprili Madagascar ilikumbwa na maandamano yaliyosababisha maafa makubwa dhidi ya sheria mpya za uchaguzi ambazo zingeliweza kuzuia aliyekuwa rais wa nchi hiyo Marc Ravalomanana kuwania katika uchaguzi wa urais, kwa mujibu wa wafuasi wake.

Mnamo Aprili 25, wabunge wa upinzani waliomba Mahakama ya Juu nchini humo kumtaka rais Rajaonarimampianina ajiuzulu sababu hakuweka Mahakama Kuu ya Sheria katika kutatua migogoro ya kisiasa.

 

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana