Pata taarifa kuu
DRC-UTALII-USALAMA

Mbunga ya wanyamapori ya Virunga yafungwa hadi mwaka 2019

Shirika la kitaifa linaloshughulikia maswala ya utalii nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ICCN limesema kuwa limesitisha Shughuli za Utalii ndani ya Mbuga ya wanyamapori ya Virunga hadi mwaka ujao.

Moja ya sehemu za kuingilia katika Hifadhi ya Taifa ya Wanayamapori ya Virunga karibu na Rutshuru tarehe 17 Juni 2014 (picha ya pikumbukumbu).
Moja ya sehemu za kuingilia katika Hifadhi ya Taifa ya Wanayamapori ya Virunga karibu na Rutshuru tarehe 17 Juni 2014 (picha ya pikumbukumbu). Junior D. Kannah / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya kufunga Mbuga hii inakuja siku chache baada ya kushuhudiwa visa vya utekaji nyara katika Hifadhi hiyo ambayo ni kivutio kwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mei 11, 2018 watali wawili kutoka Uingereza walitekwa nyara, kabla ya kuachiwa baada ya jeshi la DRC, kuendesha operesheni kabambe ya kuwaokoa watu hao kutoka mikono ya watekaji nyara.

Wakati huo mwanamke mmoj, mlinzi wa mbuga hiyo, aliyekua akiwalindia usalama, aliuawa.

Awali Mbuga ya Wanyamapori ya Virunga ilifungwa kwa muda, na ilikua inatazamiwa kufunguliwa Jumatatu wiki hii, amesema mkurugenzi wa mbuga hiyo katika taarifa yake.

"Watalii wawili na na kuuawa kwa mmoja wa walinzi wetu, ndiyo sababu tumechukua hatu ya kufunga mbunga hii. Tunahitaji kupitia utaratibu wetu wa usalama na kupata majibu sahihi, " amesema Pasteur Cosma Wilungula, Mkurugenzi wa shirika la kitaifa linaloshughulikia maswala ya utalii nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,(ICCN)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.