Pata taarifa kuu
ANGOLA-RWANDA-UBELGIJI-USHIRIKIANO

João Lourenço na Paul Kagame wafanya ziara ya kiserikali Brussels

Baada ya kufanya ziara ya kikazi nchini Ufaransa ambapo kila mmoja alipokelewa kwa muda uliopangwa, marais wa Angola João Lourenço na Paul Kagame wa Rwanda wanakutana tena wiki hii mjini Brussels kwa ziara ya kiserikali.

Rais wa Rwanda Paul Kagame, hapa ilikua Mei 2018.
Rais wa Rwanda Paul Kagame, hapa ilikua Mei 2018. Fabrice COFFRINI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kila mmoja anafanya ziara yake kwa muda uliopangwa, na watapokelewa kwa nyakati tofauti, ingawa katika mikutano ya nchi hizi mbili na Ubelgiji bila shaka kutaangaziwa mazungumzo mapya kuhusu mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini DRC. Mjini Brussels, wawili hawa kutoka Afrika watapokelewa na Mfalme wa Ubelgiji.

Balozi wa Angola mjini Brussels amethibitisha taarifa hii, huku akibaini kwamba kipaumbele cha ziara hii ya kwanza ya kiserikali ni uwekezaji. Baada ya mazungumzo na mfalme, João Lourenço anatarajia kukutana na wajasiriamali 60 wa Ubelgiji Jumatatu wiki hii. Kesho atakuwa Anvers kukutana kwa mazungumzo na wauzaji wa almasi na kutembelea bandari ya mji huo.

Kwa upande wake, Paul Kagame, aliyealikwa Brussels kushiriki katika Siku maksusi za Maendeleo ya Ulaya, pia atapokelewa na mfalme wa Ubelgiji.

Suala la mgogoro wa DRC litaangaziwa katika mazungumzo hayoo. Suala hili ni muhimu kwa majirani hawa wawili kutoka mashariki na magharibi. Tutakumbusha "umuhimu wa kuheshimu ahadi zilizotolewa na wananchi wa DRC," anasema mwanadiplomasia kutoka Angola, kama suala la "kuandaa uchaguzi mwishoni mwa mwaka huu". ameongeza mwanadiplomasia huyo. Hakuna mazungumzo yanayoendelea kati ya Angola na Rwanda kuhusu DRC, wala njama. Jambo ambalo limeikera serikali ya DRC, baada ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kutangaza kuunga mkono : jitihada za kikanda zilizopendekezwa na Umoja wa Afrika kwa kuunga mkono Angola kwa kutafutia suluhisho mgomgoro wa DRC unaoendelea.

Serikali ya DRC imekua ikishtumu Rwanda kuiba rasilimali zake kupitia mashariki mwa nchi hiyo na hivyo kuliangalia suala hili kama tishio kwa usalama wa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.