Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-HAKI-SIASA

Kiongozi wa upinzani aliyehukumiwa kifo Ethiopia aachiliwa huru

Serikali ya Ethiopia imemuachilia huru, mwanasiasa mkongwe aliyehukumiwa kifo baada ya kukamatwa nchini Yemen na kurudishwa nchini humo mwaka 2014.

Mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa, ambako wanasiasa kadhaa wa upinzani na wanaharakati wa haki za binadamu wameachiliwa huru.
Mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa, ambako wanasiasa kadhaa wa upinzani na wanaharakati wa haki za binadamu wameachiliwa huru. ©GettyImages
Matangazo ya kibiashara

Andargachew Tsige, ambaye pia ana uraia wa Uigereza, ni miongoni mwa mamia ya wafungwa wa kisiasa walioachiliwa huru wiki iliyopita.

Shirika la Utangaza la Taifa nchini humo linasema wanasiass na wanaharakati zaidi ya 500 wa upinzani wameachiiwa huru kwa sababu ya maridhiano nchini humo.

Andargachew Tsige alihukumiwa bila ya kuwepo mahakamani mwaka 2009 kwa kuhusika kwenye kundi la Ginbot 7, ambapo alikamatwa nchini Yemen miaka mitano baadaye na kusafirishwa kwenda Ethiopia.

Andargachew alihudumu kama katibu mkuu kwa kundi la kuipinga serikali ambalo lilijiita kundi la mabadiliko lakini lililotajwa na serikali ya Ethiopia kuwa kundi la kigaidi.

Mwanasheria mkuu Berhanu Tsegaye alisema Jumamosi kuwa Andargachew alikuwa ameachiliwa chini ya misingi maalum pamoja na wafungwa wengine 575.

Maelfu ya wafungwa wakiwemo wanasiasa kadhaa wa vyeo vya juu wa upinzani wameachiliwa tangu Januari baada ya kulaumiwa kwa mashtaka tofauti kadhaa yakiwemo ugaidi na uchochezi wa kuipindua serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.