Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Korea Kaskazini yarejea kwenye muungano wa Korea mbili (Seoul)
Afrika

Viongozi wa Libya wakutana Ufaransa kujadili hali ya kisiasa

media Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj (kushoto) na Jenerali Khalifa Haftar, kiongozi wa kikosi kinachoitwa Jeshi la Taifa la Libyan (ANL), wakisabahiana mbele ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron huko Celle-Saint-Cloud, karibu na Paris, Julai 25, 2017. REUTERS/Philippe Wojazer

Mkutano wa kimataifa kuhusu Libya chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa unafanyika Jumanne hii, Mei 29 katika ikulu ya Elysee ili kufungua njia ya uchaguzi kabla ya mwisho wa mwaka.

Ufaransa inataka mkutano huo kuwa hatua mpya katika mchakato wa mazungumzo ya kuondokana na mgogoro wa Libya baada ya kufaulu kukutanisha Waziri Mkuu Fayez al-Sarraj na Khalifa Haftar mnamo mwezi Julai mwaka jana. Mbali na wahusika hawa wawili, wahusika wakuu wengine wawili wa Libya wanatarajia kushiriki mkutano huo wa Paris: Aguila Saleh, Spika wa Bunge na Khaled al-Mishri, rais wa Baraza Kuu la Nchi. Wote wanatarajiwa kutia saini mkataba unaohusu uchaguzi.

Ufaransa unaweka mkutano huu katika muendelezo wa mkutano uliofanyika mnamo mwezi Julai mwaka jana kati ya Khalifa Haftar, kiongozi anayetawala mashariki mwa Libya, na Fayez al-Sarraj, Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Wajumbe wanne kutoka Libya wamealikwa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. Wanaongozwa na Fayez al-Sarraj, Waziri Mkuu wa Serikali ya Muungano wa Kitaifa; Khalifa Haftar, mkuu wa jeshi la kitaifa la Libya, mwenye makao yake makuu mashariki mwa nchi; Khaled al-Mishri, rais wa Baraza Kuu la Nchi; Aguila Saleh, Spika wa Bunge.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ambaye ni mwenyeji wa mkutano huu akishirikiana na maafisa wa Umoja wa Mataifa, wanatarajiwa kuwashawishi wanasiasa hao kukubaliana na kushiriki katika Uchaguzi wa kidemokrasia.

Hata hivyo, wadadisi wa sisa za Libya wanaona kuwa haitakuwa rahisi kuwashawishi wanasiasa hao kwa sababu sio kila mtu angependa kufanyika kwa uchaguzi huo wa wabunge na urais kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Pointi nane kuhusu uchaguzi kujadiliwa

Kwa mujibu wa taarifa zetu, Nakala ya mkataba huu mpya wa kisiasa baina ya Walibya unahusu pointi nane kuhusu kalenda na mazingira ya kufanyika kwa uchaguzi kabla ya mwisho wa mwaka huu, kwa mujibu wa kalenda itakawakilishwa na Ghassan Salameh, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Libya, kwa ushirikiano na Waziri Mkuu Fayez al-Sarraj.

Nakala hii itasayiniwa na pande za wadau kutoka Libya ambao watashiriki mkutano huo. Pande hizo zitajikubalisha kuimarisha usalama wa mchakato wa uchaguzi, kwa masharti ya kuwekewa vikwazo vya kimataifa kwa kosa la kuharibu au kuzuia mchakato huo wa uchaguzi. Uchaguzi huu unachukuliwa na Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa kama njia pekee ya kuondokana na mgogoro wa Libya.

Suala la uungwaji mkono wa majadiliano yaliyofanyika Cairo kwa minajili ya kuunganisha jeshi la Libya pia limetajwa katika ajenda ya mazungumzo hayo. Mkataba huu pia unaunga mkono kuunganishwa kwa taasisi zote za serikali, ikiwa ni pamoja na benki kuu. Hatimaye, kwa mujibu wa Ufaransa, kiongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa atauungwa mkono kwa juhudi zake kufanyika kwa Uchaguzi huu mkuu.

Karibu Walibya milioni 2.7 tayari wamejiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura, lakini rasimu ya mkataba wa Paris inataja kufunguliwa upya kwa ofisi za kujiandikisha kuhusu orodha ya uchaguzi kwa kipindi cha ziada cha siku 60.

Kwa upande wa kura ya maoni kuhusu Katiba, imepangwa kufanyika baada ya uchaguzi na sio kabla. Ufaransa inasema, kupinga Katiba kabla ya uchaguzi itaweza kuvuruga kufanyika mchakato wa uchaguzi. Kwa kusubiri, pande husika zimetakiwa kutambua Katiba ya sasa.

Hatimaye, mkutano mpya utaandaliwa ndani ya miezi mitatu ili kufuata matokeo ya makubaliano ya leo.

Kwa upande wa kimataifa, nchi ishirini na taasisi mbalimbali zinawakilishwa, nyingi katika ngazi ya mabalozi kama China, Urusi, Marekani na Uingereza. Lakini nchi za Kiafrika na majirani wa Libya zimetuma wawakilishi wa ngazi ya juu.

Chad, Niger, Congo-Brazzaville na Tunisia zitawakilishwa na marais wao. Algeria imetuma Waziri Mkuu Ahmed Ouyahia, Morocco itawakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje Nasser Bourita. Kwa upande wa Misri, itawakilishwa na Ibrahim Mahlab, Mshauri wa rais katika miradi ya kimkakati, na Hamdi Loza, Naibu Waziri wa Mambo ya Afrika.

Libya imeendelea kukosa amani, huku wanajeshi wa serikali wakiendelea kupambana na makundi ya waasi tangu kuuawa kwa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana