Rais wa Mali atangaza rasmi kuwania katika uchaguzi ujao
Rais wa Mali ametangaza rasmi kwamba atagombea tena urais kwa muhula wa tatu katika uchaguzi mkuu ambao umepangwa kufanyika tarehe 29 mwezi julai mwaka huu, na hivyo kujiunga na wagombea wengine ishirini kwenye nafasi hiyo.
Imechapishwa:
Rais Ibrahim Boubacar Keita ametoa tangazo hilo kwenye televisheni ta taifa, akisema kuwa amechukua uamuzi huo kutokana na kile anachosema kuwa amefanikiwa kuimarisha uchumi wa taifa.
"Ninatangaza kwamba nitagombea tena urais kwa muhula wa tatu katika uchaguzi mkuu ambao umepangwa kufanyika tarehe 29 mwezi julai mwaka huu."
Rais Keita ameelezea kwa nini ameamua kugombea tena urais kwa muhua wa tatu wa miaka mitano: "Ninaamua kuendelea na kazi yangu ya kutumikia vizuri Mali, wakati huu ambapo hofu na mashaka kwa wananchi bado vinatawala kutokana na kudorora kwa usalama. "
Rais Keita amesifu kazi kubwa aliofanya hasa vita dhidi ya ugaidi, huku akibaini kwamba amiimarisha jeshi lake na kulipa uwezo wa kutosha katka kulinda usalama a raia, huku akisifu pia kwa njia moja ama nyingine alivyochangia kwa kiasi kikubwa ili kufikia makubaliano ya amani na maridhiano kutokana na mchakato wa Algiers. "
Katika hotuba yake ya dakika 14, Ibrahim Boubacar Keïta amesema kuwa alisikia malalamiko kutoka kwa wananchi wa Mali ambao walidai kutoridhishwa na baadhi ya mambo katika utawala wangu, hasa utawala bora.
"Jitihada zimefanywa, hata hivyo, lakini hazijazaa matunda yanayohitajika. "
Depuis sa résidence de Sébénikoro, le Président Ibrahim Boubacar Keïta a fait sa déclaration de candidature à l’élection présidentielle du 29 juillet 2018. Retrouvez l’intégralité de cette déclaration diffusée au journal télévisé de ce 28 Mai 2018 sur l'ORTM pic.twitter.com/17D0Wg01ND
Presidence Mali (@PresidenceMali) 28 mai 2018