Pata taarifa kuu
UN. GUTERRES-AMANI-USALAMA

Guterres: Tunaenzi operesheni zinazofanya kazi kuwalinda watu

Katika kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 70, tangu kuanzishwa kwa operesheni za kulinda amani miaka 70 iliyopita, Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres yuko nchini Mali ambako azma ni kuonyesha mshikamano na walinda amani walioko nchini humo katika moja ya operesheni hatari zaidi za ulinzi wa amani za chombo hicho MINUSMA.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. DR
Matangazo ya kibiashara

Bwana Guterres kupitia ujumbe wake wa siku hii amesema pamoja na kutambua mchango wa wale walioko hai, kwa namna ya pekee wanatoa shukrani kwa walinda amani zaidi ya 3700 “waliolipa gharama ya uhai wao kwa kulinda wengine.”

Miaka ya hivi karibuni idadi kubwa ya wanawake wamekuwa wakitumwa katika operesheni mbalimbali za ulinzi wa amani katika Umoja wa Mataifa . Katika operesheni ya ulinzi wa amani nchini Mali, kuna wanawake 38 kutoka Burkina Faso ambao wanasaidia katika shughuli hii, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Makao makuu ya Minusma à Gao,  Mali
Makao makuu ya Minusma à Gao, Mali RFI/Olivier Fourt

“Na tunazienzi operesheni 14 zinazofanya kazi usiku na mchana kuwalinda watu na kuendeleza mchakato wa amani. Mwaka huu naitumia siku ya kimataifa ya walinda amani duniani nikiwa nchini Mali ili kuonyesha mshikamano wangu na wenzetu ambao wanakabiliwa na idadi kubwa ya majeruhi na hali tete.” Amesema Katibu Mkuu kupitia ujumbe wake.

Bwana Guterres amesema UN inapotambua umuhimu wa huduma na kujitolea kote duniani, pia inasimama kidete kuchukua hatua kwa ajili ya walinda amani- hatua za kufanya operesheni zetu kuwa salama na za ufanisi zaidi katika mazingira ya leo yenye changamoto.

Pia amesema wamejizatiti “kuimarisha jukumu muhimu ambalo vikosi vyetu vinastahili kulitekeleza katika kuchagiza haki za binadamu na kukabiliana na unyanyasaji na ukatili wa kingono.”

Katibu Mkuu amehitimisha ujumbe wake akisema kuwa ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa ni thibitisho la uwekezaji wa amani, usalama na ustawi duniani na kwamba, “kwa pamoja, hebu tuahidi kufanya kila tuwezalo ili kufanikisha mpango huo.”

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.