Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-SIASA-USALAMA

Mahakama ya Juu yamtaka rais wa Madagascar kuteua waziri mkuu mpya

Mahakama Kuu ya Katiba imetoa agizo kwa rais wa Madagascar kufuta serikali yake na kumteua waziri mkuu mpya anayeungwa mkono na vyama vyote vya kisiasa nchini humo.

Rais wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina.
Rais wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina. REUTERS/Lintao Zhang
Matangazo ya kibiashara

Mahakama hiyo ilielezea uamuzi wake siku ya Ijumaa kwa kushindwa kwa Rais Hery Rajaonarimampianina kuweka Mahakama Kuu ya sheria ili kutoa uamuzi kuhusu uhalifu uliotekelezwa na viongozi kadhaa wa kisiasa.

"Rais wa Jamhuri anatakiwa kufuta serikali yake na kuteua waziri mkuu mpya ndani ya siku saba tangu kuchapishwa kwa uamuzi huu kwenye orodha ya majina matatu" Mahakama Kuu ya Katiba imesema katika taarifa yake.

Mnamo mwezi Aprili Madagascar ilikumbwa na maandamano yaliyosababisha maafa makubwa dhidi ya sheria mpya za uchaguzi ambazo zingeliweza kuzuia aliyekuwa rais wa nchi hiyo Marc Ravalomanana kuwania katika uchaguzi wa urais, kwa mujibu wa wafuasi wake.

Kutokana na maandamano hayo, Hery Rajaonarimampianina alikubali kuondoa ibara hizo kwenye sheria za uchaguzi.

Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Katiba inataka rais wa nchi kushauriana na vyama vingine vya siasa vinavyowakilishwa bungeni kabla ya kuteua waziri mkuu mpya.

Mnamo Aprili 25, wabunge wa upinzani waliomba Mahakama ya Juu nchini humo kumtaka rais Rajaonarimampianina ajiuzulu sababu hakuweka Mahakama Kuu ya Sheria katika kutatua migogoro ya kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.