Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

DRC: Watu 22 ndio walifariki kutokana na Ebola badala ya 27

Kesi zaidi ya 50 za maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola na vifo 22 vimeripotiwa kaskazini-magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kulingana na ripoti mpya ya serikali ya DRC iliyotolewa Ijumaa wiki hii, na hivyo kupunguza idadi ya awali, ambapo ilidaiwa zaidi ya watu 27 walifariki dunia.

Gari la wagonjwa likimsafirisha mgonjwa wa Ebola, Mbandaka tarehe 22 Mei 2018.
Gari la wagonjwa likimsafirisha mgonjwa wa Ebola, Mbandaka tarehe 22 Mei 2018. AFP -Junior D. Kannah
Matangazo ya kibiashara

"Kwa jumla, kesi 52 za maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola zimeripotiwa katika jimbo hilo, ikiwa ni pamoja na 31 ambazo zimethibitishwa, 13 ambzo zina dalili ya ugonjwa huo na 8 ambazo zinashukiwa kuwa na dalili ya ugonjwa huo" , imesema taarifa ya Wizara ya Afya ya DRC.

Idadi ya vifo ni watu 22, wizara ya Afya imebaini, huku ikipunguza idadi kesi za maambukizi (kutoka 58 hadi 52) na idadi ya vifo (kutoka 27 hadi 22).

Kwa upande wa serikali ya DRC, tofauti hii inaelezwa na ukweli kwamba vifo vingine vilidaiwa kimakosa kuwa vilisababishwa na Ebola, wakati ambapo baadhi ya kesi, kwenye vipimo vya maabara, hazikuonyesha dalili zozote za virusi vya Ebola.

Mlipuko wa Ebola ulizuka Machi 8 katika eneo la Bikoro, kilomita 600 kaskazini mwa mji mkuu wa DRC, Kinshasa. Halafu uliendelea kuenea kwa mji wa Mbandaka, ulio na watu milioni 1.2.

Kampeni ya chanjo inayolenga wafanyakazi wa afya ambayo ilianza tangu Jumatatu wiki hii, imekua ikiendelea nchini humo tangu Jumatatu.

Shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Watoto (Unicef) limehakikisha kwamba limejitolea kwa watoto wa shule katika kupambana dhidi ya kuenea kwa janga la Ebola katika jimbo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.