Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-TAIWAN-USHIRIKIANO

Burkina Faso yavunja uhusiano wa kidiplomasia na Taiwan

Nchi ya Burkina Faso imevunja uhusiano na Taiwan, ambayo imekua ikitoa msaada muhimu kwa nchi hii kutokana na msaada wake wa kidiplomasia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso, Alpha Barry, ametangaza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso, Alpha Barry,
Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso, Alpha Barry, CRÉDITISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Serikali ya Burkina imeamua leo kuvunja husiano wa kidiplomasia na Taiwan," amesema Barry katika taarifa yake.

"Tangu mwaka 1994, Burkina Faso imekua na uhusiano wa ushirikiano na Taiwan. Lakini leo, changamoto mbalimbali za kidunia, changamoto za kiuchumi na kijamii za nchi yetu na ukanda huu zinapendekeza tufikiria upya msimamo wetu," Bw Barry amebaini.

"Uamuzi huu umechukuliwa kwa nia njema ya kutetea maslahi ya Burkina Faso na raia wake katika mzunguko mzima wa mataifa na kujenga ushirikiano bora katika kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi yetu na kuwezesha miradi ya kikanda " ameongeza waziri huyo.

"Rais wa Burkina Faso Roch Marc Christian Kaboré ameniagiza kama Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano kuchukua hatua zote zinazohitajika kwa kufunga ubalozi wetu Taipei na ule wa Taiwan katika nchi yetu," amesema Bw Barry.

Tangu mwaka wa 2000, nchi kadhaa za Afrika ikiwa ni pamoja na Chad na Senegal, ambazo zilikua zikipata misaada kutoka Taiwan, zilivunja uhusiano na nchi hiyo kwa minajili ya kupata msaada kutoka ushirikiano na China, ambayo inazitaka nchi za kiafrika na nyinginezio kujitenga mbali na Taiwan.

Kwa hatua hii ya Burkina Faso, Swaziland pekee miongoni mwa nchi za Afrika ndio bado inaendelea na uhusiano na Taiwan.

Leo, nchi 18 pekee, ikiwa ni pamoja na Vatican na mataifa ya Pacific na Amerika ya Kusini (Honduras, Guatemala na Kiribati), yanaendelea kutambua kisiwa hiki cha Taiwan kilichojitenga na China tangu mwaka 1949. Kabla ya Burkina Faso, Jamhuri ya Dominika pia ilitangaza kuvunja uhusiano na Taiwan mnamo Machi 1.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.