Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

Kesi mbili mpya za ugonjwa wa Ebola zaripotiwa DRC

Kesi mbili mpya za ugonjwa wa Ebola zimeripotiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Wizara ya Afya ya nchi hiyo imetangaza Jumanne wiki hii. Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na Ebola, inaendelea kuongezeka wakati chanjo dhidi ya ugonjwa huo ilianza kutolewa Jumatatu wiki hii.

Watu wawili wafariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)
Watu wawili wafariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Mmoja miongoni mwa wawili hao waliofariki kutokana na ugonjwa wa Ebola alikuwa katika mji wa Mbandaka (wenye wakazi milioni 1.2), ambao unatembelewa na wasafiri wengi wanaotumia njia ya bahari, nchi kavu na angani kuelekea au kutoka mji mkuu, Kinshasa.

Mwathirika mwingine, ambaye ni muuguzi, amefariki katika kijiji cha Bikoro, kaskazini magharibi mwa nchi, ambapo mlipuko wa Ebola uligunduliwa, Jessica Ilunga, msemaji wa wizara ya Afya ameliambia shirika la habari la Reuters.

Vifo vilivyosababishwa na ugonjwa wa Ebola vimeongezeka mpaka kufikia 27, kwa mujibu wa chanzo cha hospitali.

Kesi saba mpya zimeripotiwa katika sekta ya Bikoro, Wizara hiyo imesema.

Mamlaka za afya ambazo zina matumaini ya kudhibiti kusabaa kwa ugonjwa huo, kwa ushirikiano na shirika la Afya Duniani walianzisha kampeni ya kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo hatari wa Ebola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.