Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-SIASA-USALAMA

Umoja wa Mataifa washindwa kuanzisha mazungumzo Madagascar

Kwa karibu mwezi mmoja sasa, Madagascar imekumbwa na mgogoro wa kisiasa ambao inaonekana umeshindwa kutafutiwa suluhu. Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Abdoulaye Bathily aliondoka Madagascar Jumatano wiki hii (Mei 16) na wawakilishi wa SADC. Maswali yameibuka kuhusu mchango wa Jumuiya ya kimataifa kuhusu usuluhishi huu.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Abdoulaye Bathily.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Abdoulaye Bathily. AFP PHOTO / MARCO LONGARI
Matangazo ya kibiashara

Baada ya wawakilishi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya mwishoni mwa wiki iliyopita, ilikuwa ni zamu ya Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kuondoka katika kisiwa hiki kikuu siku ya Jumatano.

Hata kama walikaa muda mrefu, hawakuweza kufikia makubaliano mazuri ya kisiasa ambayo yanaweza kuiondoa nchi hiyo katika mgogoro huo. Makubaliano ambayo yataweza kukamilisha mazungumzo kati ya rais wa nchi hiyo na viongozi wa vyama vya upinzani Marc Ravalomanana na Andry Rajoelina.

Katika taarifa zilizotolewa na Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, waliwahimiza wawakilishi wa kisiasa wa Madagascar kuendelea na mazungumzo. Na kusisitiza kwamba uchaguzi utafanyika kulingana na kanuni za kikatiba.

Maswali ambayo yanatakiwa kujadiliwa ni pamoja na heshima ya uhalali na Katiba, serikali ya makubaliano na kubaki kwa rais mamlakani.

Wabunge wa upinzani wanasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu ya Katiba kwa ombi la kuondoka kwa rais wa nchi hiyo, ambapo upande wa utetezi unatarajiwa kutoa msimamo wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.