Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Hali ya wasiwasi yazuka kwenye msikiti ulioshambuliwa Durban

media Polisi kwenye lango wa msikiti ambapo watu wasiojulikana walishambulia waumini kwa visu, katika mji wa Durban, Mei 10, 2018. Imam aliuawa na watu wawili walijeruhiwa vibaya. RAJESH JANTILAL / AFP

Nchini Afrika Kusini, polisi iligundua bomu siku ya Jumapili usiku, Mei 13, katika msikiti mmoja kaskazini mwa Durban. Msikiti huo ulivamiwa na watu wasiojulikana ambao walishambulia waumini kwa visu.

Mtu mmoja aliuawa na wengine wawili walijeruhiwa. Hii ni mara ya pili ndani ya siku chache msikiti huu ukilengwa kwa mashambulizi. Polisi imefutilia mbali dhana ya shambulio la kigaidi.

Waumini wa Msikiti huo wanasema waliona kitu kama bomu kabla ya kuanza sala yao hapo jana na kuwaita maafisa wa Polisi ambao walithibitisha kuwa ni bomu.

Hali hii imezua wasiwasi nchini humo baada ya kubainika kuwa mahubiri ya itikadi kali yamekuwa yakifunzwa katika msikiti huo ulio katika mji wa Pwani wa Durban.

Ripoti zinasema kuwa, msikiti huo umefungwa kwa muda ili kuruhusu ucungunguzi wa tukio hilo.

Licha ya kifo cha mtu na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kuvamiwa, hakuna yeyote aliyekamatwa.

Kiongozi mmoja wa dini hiyo ya Kiislamu amesema, msikiti huo ulilengwa kwa sababu ilikuwa inaegemea Waislamu wenye kutoka dhehebu la Shia.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana