Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

DRC: Zoezi la kutambua miili iliyopatikana Kasaï laendelea

media Wataalam wa Umoja wa Mataifa Zaida Catalan (picha ya mwaka 2009) na Michael Sharp waliuawa katika mji wa Kasai mnamo mwezi Machi 2017. BERTIL ERICSON, TIMO MUELLER / TT News Agency / AFP

Katika sehemu ya operesheni ya kutafuta wasaidizi wa wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa waliouawa mnamo mwezi Machi 2017 wakati ambapo walikua wakifanya uchunguzi kuhusu vurugu huko Kasai, katikati mwa DRC, serikali imethibitisha kwamba imepata miili minne. Vipimo vya DNA vinaendelea.

Hii ni hatua inayoendelea katika uchunguzi kuhusu mauaji ya wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa huko Kasaï na kutoweka kwa wasaidizi wao, raia wa DRC, mnamo mwezi Machi 2017.

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imethibitisha kwamba imegundua miili minne ambayo inaweza kuwa ya wasaidizi hao wa wataalam wa Umoja wa Mataifa waliouawa.

Vipimo vya DNA vinaendelea ili kuweka majina kwenye miili ya waathirika, Mushobekwa Marie-Ange, Waziri wa Haki za Binadamu ameiambia RFI.

"Mamlaka za DR Congo zinaendelea kushirikiana na Umoja wa Mataifa ili kutoa mwanga kwa kile kilichotokea Kasai na waathirika wote wa Kamuina Nsapu watatndewa haki, " amesema Marie-Ange Mushobekwa.

"Ni kazi ambayo madaktari husika watafanya kuthibitisha kuwa miili iliyopatikana ni kweli miili ya wasaidizi wa wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa waliouawa"

Kwa upande wa serikali ya DR Congo, wanamgambo wa Kamuina Nsapu wanahusika katika mauaji ya wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa, Michael J. Sharp, Mmarekani, na raia wa Sweden, Zaida Catalan, waliouawa kikatili karibu na Bunkonde katika jimbo la Kasai ya Kati mnamo mwezi Machi 2017, baada ya kuzuka uasi wa wafuasi wa kiongozi wa Kamuina Nsapu. Tangu wakati huo, wasaidizi wa wataalam hao, Betu Tshintela, Isaac Kabuayi na Pascal Nzala bado hawajulikani walipo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana