Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Suala la raia wa DRC waishio ugenini kushiriki mchakato wa uchaguzi lazua mjadala

media Zoezi la sensa kwa raia wa DRC watakaoshiriki uchaguzi limepangwa kufanyika Julai 1 hadi Septemba 28, 2018. Government of the Democratic Republic of the Congo / Wikimedia

Mchakato wa uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umeendelea kuibua maswali mengi kuhusu raia wa nchi hiyo waishio ugenini kushiriki uchaguzi. Zoezi la sensa kwa raia hao limepangwa kuanza Julai mosi hadi Septemba 28, kulingana na kalenda ya Tume ya Huru ya Kitaifa Uchaguzi (Ceni).

Baadhi ya wajumbe wa mashirika ya kiraia na wengine kutoka upinzani wana hofu kuwa huenda kukawa na njama katika zoezi hilo kutumiwa kwa kuwaruhusu raia hao kushiriki mchakato wa uchaguzi ili kuahirisha uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba 2018.

Tume ya Uchaguzi (Ceni) inasema kuwa iko tayari kwa zoezi la kuandikisha raia waishio ugenini kwa muda uliotolewa na kalenda ya uchaguzi.

Wakati wa mkutano na Spika wa Bunge Aubin Minaku mwezi Mei, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Corneille Nangaa aliwasilisha hali ya maandalizi ya operesheni hii. Alimwambia kuwa vifaa vya uchaguzi 220 vimeandaliwa, vimewekwa na viko tayari kutumwa katika maeneo husika. Pia aliongeza kuwa maeneo ya kufanyia zoezi la kuandikisha raia hao pia yamejulikana.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi alichukua fursa hiyo kwa kuwasilisha changamoto zinazohusiana na utekelezaji wa operesheni hii. Hasa, kuna ugumu wa kujua kama raia watakaoshiriki zoezi hilo wana utaifa wa Congo kama inavyotakiwa na sheria. Lakini pia suala la usalama, kutokana na kwamba baadhi ya raia wa DRC waishio ugenini wakati mwingine huwa na vurugu kwa wawakilishi wa taasisi za sasa.

Katika upande wa upinzani, mbunge wa chama cha UNC Juvenal Munubo amesema kuna ulazima wa kuweka wazi lengo kuu la mchakato huu, ambalo alisema kuwa uchaguzi wa urais unapaswa kufanyika mnamo Desemba 2018. Amesema ikiwa zoezi hilo litakuja kuvuruga mchakato wa uchaguzi, afadhali lisimamishwe.

"Jambo muhimu zaidi kuliko yote, "ni uchaguzi wa Desemba 23, 2018, " amesema mbunge Munubo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana