Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Korea Kaskazini yarejea kwenye muungano wa Korea mbili (Seoul)
Afrika

Jamhuri ya Afrika ya kati yaomboleza vifo vya watu 24 waliouawa

media Rais wa Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra katika mkutano na waandishi wa habari tarehe 11 Aprili 2018 huko Bangui, baada ya mapigano katika wilaya ya PK5 kati ya Minusca, vikosi vya usalama vya ndani na makundi ya wanamgambo. FLORENT VERGNES / AFP

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya kati Faustin Archange Touadera ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo vya watu wasiopungua ishirini na wanne waliouawa katika mapigano kati ya wapiganaji wenye silaha na vikosi vya serikali.

Mapigano hayo yalitokea katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui ambapo kanisa Notre Dame lilishambuliwa pia.

Tume ya umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCA imesema imeimarisha doria kwenye mji mkuu Bangui na hasa wilaya ya PK5 ambayo imekuwa kitovu cha vurugu za kidini na umiliki wa maeneo wa makundi ya wapiganaji.

Mapigano haya yanazusha maswali zaidi kuhusu uimara wa serikali ya nchi hiyo na uwepo wa vikosi vya MINUSCA.

Machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yamesababisha vifo vya watu wengi na maelfu wengine kulazimika kuyahama makazi yao.

Wadadisi wanasema kuwa vita hivyo vinachochewa kidini, lakini kuna mwingiliano wa kisiasa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana