Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Korea Kaskazini yarejea kwenye muungano wa Korea mbili (Seoul)
Afrika
CAR

Machafuko yaongezeka Bangui, kanisa Notre-Dame lashambuliwa

media Mlipuko wa gruneti mbele ya mlango wa kanisa Notre-Dame de Fatima huko Bangui wakati wa shambulio la mwaka 2014 (picha ya kumbukumbu). MARCO LONGARI / AFP

Mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui, unaendelea kukabiliwa na mdororo wa usalama. Machafuko yameendelea kuongezeka katika maeneo mbalimbali ya mji huo. Kanisa Notre Dame, lililo karibu na kata ya PK5, lililishambuliwa Jumanne wiki hii na kundi la watu wenye silaha wakati waumini walikua wakishiriki misa.

Watu 16 waliuawa katika shambulizi hilo na 99 kujeruhiwa kwa mujibu wa shirika la Msalama Mwekundu nchini humo.

Machafuko hayo yameanza kuzua hofu kwa raia kuwa huenda machafuko yakaongezeka zaidi ikilinganishwana miaka kadhaa iliyopita. Rais wa nchi hiyo ametoa ujumbe mkali dhidi ya watu wanaohusika na machafuko hayo.

Yote yalianza Jumanne asubuhi wiki hii na tukio lililohusisha Moussa Empereur, kutoka kundi la wanamgambo la Nimery Matar Djamous almaarufu Force. Tukio ambalo mtu huyo inasadikiwa kuwa alijeruhiwa na vikosi vya usalama wa ndani. Kwa kulipiza kisasi, kundi la watu wenye silaha kutoka KM5 lilishambulia kanisa Notre-Dame de Fatima ambapo mamia ya waumini Wakatoliki walikusanyika kwa misa.

Nyuma ya kanisa kulikuwa na uzio. Walivunja na kupitia kwenye la kanisa.kwa mujibu wa shahidi aliyeshiriki misa wakati wa shambulio hilo.

Watu kadhaa waliuawa ikiwa ni pamoja na padri aliyekua anaheshimiwa sana mjini Bangui, Albert Toungoumalé-Baba. Vikosi vya usalama wa ndani vilifaulu kuzima shambulio hilo na kurejesha nyuma kundi hilo la wauaji. Waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini na katika vituo mbalimbali vya afya katika mji huo.

Watu wenye hasira waliamua kusafirisha mwili wa padri hadi ikulu. Msafara huo ulipita katika kata ya Lakouanga ambapo msikiti ulichomwa moto na watu wawili wakauawa kwa kuchamwa moto.

Hali hiyo imeendelea kushihudiwa katika maneo mbalimbali ya mji huo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana