Pata taarifa kuu
UBELGIJI-DRC-USHIRIKIANO

Ubelgiji na DRC zaendelea kulumbana

Ubelgiji imeeleza sababu za kumuita balozi wake nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya congo tangu mwezi January mwaka huu, baada ya nchi hiyo kuwa na mahusiano mabaya ya kidiplomasia na serikali ya kinshasa.

Maandamano na kundi la waumini wa kanisa Katoliki wakiomba Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila Kabange kujiuzulu, Kinshasa mnamo Februari 25, 2018.
Maandamano na kundi la waumini wa kanisa Katoliki wakiomba Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila Kabange kujiuzulu, Kinshasa mnamo Februari 25, 2018. JOHN WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji Didier Reinders alithibitisha Jumatatu wiki hii uamuzi wa Brussels wa kumrejesha nyumbani balozi wake aliyekuwa jijini Kinshasa Bertrand de Crombrugghe, akieleza kuwa mazingira ya mahusiano ya kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili hayakuwa mazuri huku akiishutumu serikali ya DRC kushindwa kuonyesha ushirikiano katika masuala mengi ikiwemo ya kijeshi lakini pia kisiasa.

Hata hivyo vyombo vya habari vya Ubelgiji hali kadhalika vyanzo vya kidiplomasia vimeripoti kuwa kulikuwa na uvunjaji wa uaminifu kati ya nchi hiyo ambayo iliitawala kikoloni DRC na serikali ya Kinshasa baada ya kutangazwa uamuzi wa kufungwa kwa ubalozi mdogo wa shengen, hatua ambayo ilionekana kuchochea uhasama zaidi.

Balozi Bertrand de Crombrugghe kwa upande wake amesema kuwa Wizara ya mambo ya nje ya Ubelgiji ilishangazwa na hatua ya Kinshasa baada ya yeye kupokea barua ya kumtaka aondoke nchini humo.

Kufwatia hatua hiyo Ubelgiji iliamua kusitisha uhusiano wake wa kijeshi na hivyo kuitisha nyumbani wakufunzi wake, maafisa wa kijeshi, waliokuwa huko DRC kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa FARDC.

Ubelgiji imekuwa ikiitaka serikali ya Kinshasa kuboresha mazingira ya kisiasa na kuhakikisha makubaliano yaliyosainiwa chini ya upatanisho wa kanisa Katolijki CENCO yanatekelezwa, na uchaguzi unafanyika chini ya misingi ya kidemokrasia nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.