Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-SIASA-USALAMA

Mazungumzo ya kuondokana na mgogoro wa kisiasa yaanza Madagascar

Mazungumzo yameanza mjini Antananarivo kati ya chama tawala na upinzani ambao umekuwa ukiandamana tangu siku ya Jumamosi wiki iliyopita na kutoa wito kwa Rais Hery Rajaonarimampianina kujiuzulu miezi michache kabla ya Uchaguzi mkuu.

Madagascar, mkutano wa upinzani uliosambaratishwa vibaya na polisi, kwenye makao makuu ya jiji,  Antananarivo, tarehe 21 Aprili 2018.
Madagascar, mkutano wa upinzani uliosambaratishwa vibaya na polisi, kwenye makao makuu ya jiji, Antananarivo, tarehe 21 Aprili 2018. RIJASOLO / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Mkutano wa mazungumzo umefanyika kati yetu na wapinzani jana (Jumatano) jioni katika makao makuu ya Umoja wa Afrika" mjini Antananarivo, kiongozi wa chama cha tawala cha HVM, Rivo Rakotovao, amesema.

Majadiliano kati ya wabunge wa upinzani na Bw Rakotovao mwenyewe yanatarajiwa kuanza Alhamisi wiki hii saa 12 jioni saa za Madagascar, Bw Rakotovao ameongeza, bila kutoa maelezo kuhusu mazungumzo hayo.

"Jumuiya ya kimataifa kupitia Umoja wa Afrika umealika wadau katika mgogoro huo kuketi kwenye meza ya mazungumzo," amesema Augustin Andriamananoro, mshirika wa karibu wa Andry Rajoelina, mmoja wa viongozi wa upinzani.

"Umoja wa Afrika unatafuta njia ya upatanisho ili kuondokana na mgogoro huo mara moja," ameongeza.

Mgogoro huu mpya nchini Madagascar, kisiwa kikubwa katika Bahari ya Hindi chenye historia ya kisiasa yenye utata, ulianza siku ya Jumamosi kwa maandamano ya upinzani ambayo yalisababisha makabiliano na polisi. Watu wawili waliuawa.

Upinzani ulitoa wito wa kuandamana kupinga sheria mpya za uchaguzi ambazo zinaonekana kuwa kuegemea upande wa serikali.

Tangu wakati huo, maandamano yanaendelea kila siku katika mji mkuu wa nchi hiyo, kwa kauli mbiu mpya: kupata hakikisho la kujiuzulu kwa rais, madarakani tangu mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.