ZIMBABWE-SIASA-HAKI
Zimbabwe yajiandalia uchaguzi
Mahakama maalum zimeundwa nchini Zimbabwe ili kusikiliza na kuhumu kesi kuhusu machafuko yatakayotokea baada ya kipindi cha Uchaguzi.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Uzinduzi huu umefanyika kuelekea Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Julai.
Utakuwa ni Uchaguzi wa kwanza bila ya rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe aliyetimuliwa madarakani mwaka uliopita.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa alitangaza kwamba Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwaka huu nchini Zimbabwe unapaswa kufanyika "kabla ya mwezi Julai". Tangazo hili alilitoa katika mkutano wa kiuchumi duniani uliofanyika Davos, nchini Uswisi.