Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Rais wa Angola amtimua mkuu wa majeshi

media Rais wa Angola João Lourenço. JOOST DE RAEYMAEKER/LUSA

Rais wa Angola Joao Lourenco amemfuta kazi Mkuu wa Majeshi Jenerali Geraldo Sachipengo Nunda, baada ya kutajwa katika kashfa ya ufisadi.

Kiongozi huyo aliyeingia madarakani mwezi Septemba mwaka uliopita, amekuwa akiachana na waliokuwa washirika wa rais wa zamani Jose Eduardo dos Santos aliyeongoa nchi hiyo kwa miaka 37.

Mnamo mwezi Novemba mwaka jana Lourenco alimfuta kazi kamanda wa jeshi la polisi Ambrosio de Lemos na mkuu wa upelelezi (usalama wa taifa) Antonio Jose Maria katika mabadiliko makubwa ya kwanza ya vyombo vya usalama tangu tangu alipoingia madarakani mwezi Septemba mwaka jana.

Miezi michache baadae alimfuta kazi binti wa rais wa zamani Isabel Dos Santos ambaye alikuwa mkuu wa kampuni ya mafuta nchini humo na mwanamke tajiri zaidi barani Afrika kinyume na matarajio ya wengi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana