Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
Afrika

Uhaba wa fedha wawasumbua wanajeshi wa AMISOM nchini Somalia

media Wanajeshi wa Uganda wanaopambana na Al Shabab nchini Somalia news.un.org

Mkuu wa Majeshi nchini Uganda Jenerali David Muhoozi anahofia hali ya wanajeshi wa UPDF walio nchini Somalia chini ya mwavuli wa wanajeshi wa Umoja wa Afrika AMISOM, kutokana na uhaba wa fedha kusaidia kufanikisha operesheni zake dhidi ya kundi la kigaidi la Al Shabab.

Jenerali Muhoozi ameliambia Gazeti la kila siku nchini Uganda Daily Moniter kuwa, wanajeshi wake wanashindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo wakiwa na lengo la  kuwaachia kazi kubwa wanajeshi wa Somalia.

Jeshi la UPDF lilikuwa na mpango wa kuwa na kambi mbalimbali nchini Somalia, ili kuwaacha wanajeshi wa Somalia kudhibiti maeneo yaliyokombolewa lakini ukosefu wa fedha umeendelea kuwa changamoto.

Hatua hii inaweka njia panda, ahadi ya  serikali ya Uganda kuwa iko tayari kutuma wanajeshi zaidi 5,000 nchini Somalia iwapo kutakuwa na hakikisho la kuwepo kwa ufadhili zaidi kutoka kwa Jumuiya ya Kimataifa.

Uganda ni miongoni mwa mataifa mengine ya Afrika kama Burundi, Djibouti, Ethiopia na Kenya yaliyotuma wanajeshi wake nchini Somalia kuwashinda magaidi tangu mwaka 2007.

Rais Yoweri Museveni alikuwa kiongozi wa  kwanza barani Afrika kutuma kikosi cha zaidi ya wanajeshi 6,000 kuungana na wale wapatao 22,000 kutoka mataifa hayo ya Afrika kuilinda serikali ya Mogadishu na kuwashinda magaidi.

Mwaka 2016, wafadhili wakubwa wa AMISOM ambao ni Umoja wa Ulaya,  walipunguza mshahara wa wanajeshi wanaopata  kila mwezi kutoka Dola 1,028 hadi Dola 822, kwa sababu ya changamoto za kiuchumi barani Ulaya.

Hata hivyo, baada ya miaka 10 bajeti ya Umoja wa Ulaya iliongezeka na kufikia Euro Milioni 20 kila mwezi kutokana na ongezeko la wanajeshi wa AMISOM.

Watalaam wa usalama wanaonya kuwa iwapo wafadhili wa Kimataifa hawataongeza bajeti huenda ushindi dhidi ya Al Shababa ukawa wa muda mfupi.

Mwezi Machi, marais kutoka mataifa yaliyotuma wanajeshi wake nchini Somalia, walikutana jijini Kampala na kutoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuongeza kiwango kinachotumwa kufanikisha vita dhidi ya ugaidi nchini humo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana