Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Maelfu ya wauguzi wanaogoma wafukuzwa kazi Zimbabwe

media Les policiers zimbabweens tentent de disperser les médecins et infirmiers … Polisi wa Zimbabwe wanajaribu kusambaratisha madaktari na wauguzi ambao wanaandamana wakipinga mazingira yao ya kazi, na ukosefu wa madawa. ( Photo : AFP/ Desmond Kwande )

Serikali ya Zimbabwe imetangaza kwamba imewafukuza kazi maelfu ya wauguzi wanaoendelea na mgomo wakidai kulipwa mshahara mzuri.

"Kwa maslahi ya wagonjwa na kuokoa maisha ya watu, serikali imeamua kuwafukuza kazi wauguzi wote wanaoendelea na mgomo, hatua ambayo inachukuliwa papo hapo," alisema makamu rais Constantino Chiwenga katika taarifa Jumanne wiki hii.

Bw Chiwenga amewashtumu wauguzi hao kwamba "walishawishiwa kisiasa".

Wagonjwa hawakuweza kuelekea hospitali kuu wiki hii baada ya mgomo wa wauguzi kuanza. Mgomo huo ulianza wiki kadhaa tu baada ya mgomo wa madaktari.

Makamu rais wa Zimbabwe aliongeza kuwa wauguzi wasio na ajira na wastaafu wanatajiria kuchukua nafasi ya wale waliofukuzwa kazi.Jenerali Chiwenga aliongoza operesheni ya kung'olewa kwa rais Robert Mugabe mnamo mwezi Novembea 2017 wakati jeshi lilipochukua kwa muda mfupi udhibiti wa nchi kabla kuteuliwa kwa rais Emmerson Mnangagwa.

Jenerali Chiwenga amesema anasikitishwa na mgomo wa wauguzi wakati ambapo serikali ilitoa dola milioni 17 ili kuboresha mishahara yao. Chiwenga ameongeza kwamba sasa pesa hizi zitatumika kwa kulipa mishahara ya wauguzi wapya.

Chama cha Wauguzi nchini Zimbabwe kimesema kuwa "kimepokea" taarifa ya Chiwenga lakini kitaendelea na mgomo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana