Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Mahakimu 250 wafutwa kazi DRC

media Serikali ya Kinshasa yawatimua mahakimu 250 CC/Wikimedia Commons

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewafuta kazi Mahakimu 250 ambao hawana elimu ya sheria pamoja na wale ambao walikuwa wameshtumiwa kuwa mafisadi.

Waziri wa Sheria Alexis Thambwe Mwamba amesema hatua hii imechukuliwa ili kuwazuia watu waliokuwa wanaingia katika idara ya Mahakama wakiwa na lengo la kujipatia fedha badala ya kuwatumikia raia wa nchi hiyo.

Hii sio mara ya kwanza kwa serikali ya Kinshasa kuwachukulia hatua maafisa wa juu wa idara ya Mahakama, Mwaka 2009, rais Joseph Kabila aliwafuta kazi Majaji 96 baada ya kubainika kuwa walikuwa wafisadi.

Hatua hii inakuja ikisalia miezi 7 ili kufanyike Uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 23 mwaka huu.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana