Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA-UGAIDI

Askari auawa,20 wajeruhiwa baada ya shambulizi Timbuktu nchini Mali

Shambulizi la roketi na bomu lililotegwa garini limeua Askari mmoja wa kulinda amani nchini Mali na kujeruhi wengine kadhaa wa kikosi cha Ufaransa Mjini Timbuktu nchini Mali maafisa wameeleza.

Baadhi ya wanajeshi wa Ufaransa mjini Timbuktu nchini Mali
Baadhi ya wanajeshi wa Ufaransa mjini Timbuktu nchini Mali REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Kulingana taarifa ya wizara ya ulinzi nchini Mali iliyochapishwa katika ukurasa wa FB shambulizi la kigaidi lililenga kambi ya kijeshi ya ufaransa na jeshi la UN nje ya mji wa kaskazini jumamosi mchana.

Washambuliaji wawili waliovalia kama askari wa umoja wa mataifa wakiwa na pikipiki walishambulia kwa maroketi kambi hizo mbili.

Wizara ya ulinzi nchini Mali imesema askari mmoja ndie alipoteza maisha na majeruhi kutoka jeshi la Ufaransa watano wakiwa katika hali mbaya.

Hata hivyo makabiliano yalikwisha jioni na jeshi kudhibiti hali ya usalama huku uchunguzi ukiwa umeanza.

Chanzo kimoja kutoka jeshi la kigeni kimeliambia shirika l ahabari la Ufaransa AFP kuwa shambulizi la jana lilikuwa na kushtukiza mjini timbuktu.

Awali Umoja wa mataifa nao ulitoa tawimu ya waathirika wa shambulizi hili kama ilivyobainishwa na wizara ya ulinzi ya Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.