Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/04 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/04 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Haraka
Kundi la Islamic State (IS) ladai kuhusika na mashambulizi nchini Sri Lanka bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi (Amaq)
Afrika

Buhari kuwania tena urais mwaka 2019

media Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari REUTERS /Stringer

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari wiki hii alithibitisha kuwa atawania tena urais kwa muhula wa pili mwaka 2019.

Hatua hiii inamaliza uvumi wa muda mrefu kuhusu hatima ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 75 ambaye amekuwa akisumbuliwa na afya mara kwa mara.

Buhari atawasilisha ombi kwa chama chake APC, kuomba tiketi ya chama hicho kuelekea Uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Februari mwakani.

Mwanasiasa huyo  Mwislamu kutoka Kaskazini kwa Nigeria alikuwa mwanasiasa wa kwanza wa upinzani kumshinda rais aliye madarakani wakati huo Goodluck Jonathan.

Hatima yake sasa ipo mikononi mwa chama chake ambacho kitakutana kuamua iwapo atawania tena wadhifa huo licha ya umri wake mkubwa na hali yake ya kiafya.

Buhari ambaye mara kwa mara amekuwa akizuru nchini Uingereza kupata matibabu, uongozi wake umekuwa ikipambana na ufisadi na kuimarisha uchumi wa taifa hilo la Afrika Magharibi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana