Pata taarifa kuu
TANZANIA-UFARANSA-BIASHARA

Wafanyabiashara wa Ufaransa kuwekeza katika kilimo, Usafirishaji na Teknolojia nchini Tanzania

Wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa kuwasili nchini Tanzania kuangazia fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekta za Kilimo,Teknolojia  na usafirishaji

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Claivier akiwahotubia wanawake kutoka barani Afrika wakati wa mkutano wa kuhimiza umuhimu wa wanawake kujikita katika masuala ya sayansi jijini Dar es salaam Machi 08 2018
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Claivier akiwahotubia wanawake kutoka barani Afrika wakati wa mkutano wa kuhimiza umuhimu wa wanawake kujikita katika masuala ya sayansi jijini Dar es salaam Machi 08 2018 Emmanuel Makundi/Rfi Kiswahili
Matangazo ya kibiashara

Hayo yamebainika wakati Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier akizungumzia ziara ya siku tatu ya ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa wanaokwenda nchini Tanzania kuangazia fursa za kibiashara baina ya nchi hizo mbili.

Balozi Clavier ameongeza kuwa ujumbe huo utaongozwa na Shirikisho la Kimataifa la wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa MEDEF lenye wanachama 750,000 wakilenga kuwekeza katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na katika sekta za kilimo, Teknolojia ya habari na Mawasiliano na Mafuta na Gesi.

  “Ziara hii yenye wakurugenzi 30 wa kampuni mbalimbali wanataka kushirikiana na Tanzania katika sekta za Usafiri ukiwemo wa anga na ardhini,TEHAMA,Kilimo ni miongoni mwa mengine” alisema Clavier.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Uchumi na Biashara wa Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania Beatrice Alperte amesema ukuaji wa teknolojia unakwenda sambamba na ukuaji wa uchumi kwa kuzingatia tafiti ndio maana wameamua kushirikiana na Tanzania katika kukuza uwezo wa watendaji.

Biashara kati ya Tanzania na Ufaransa imekua kwa wastani wa Dola za kimarekani milioni 30 ambapo Wafanyabiashara hao wanatarajia kukutana na Rais wa Tanzania Dkk.John Pombe Magufuli,Mawaziri katika sekta mbalimbali pamoja na viongozi wa sekta binafsi TPSF nchini.

Ripoti ya Mwandishi wa Rfi Kiswahili Steven Mumbi

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.