Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Wafanyabiashara wa Ufaransa kuwekeza katika kilimo, Usafirishaji na Teknolojia nchini Tanzania

media Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Claivier akiwahotubia wanawake kutoka barani Afrika wakati wa mkutano wa kuhimiza umuhimu wa wanawake kujikita katika masuala ya sayansi jijini Dar es salaam Machi 08 2018 Emmanuel Makundi/Rfi Kiswahili

Wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa kuwasili nchini Tanzania kuangazia fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekta za Kilimo,Teknolojia  na usafirishaji

Hayo yamebainika wakati Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier akizungumzia ziara ya siku tatu ya ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa wanaokwenda nchini Tanzania kuangazia fursa za kibiashara baina ya nchi hizo mbili.

Balozi Clavier ameongeza kuwa ujumbe huo utaongozwa na Shirikisho la Kimataifa la wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa MEDEF lenye wanachama 750,000 wakilenga kuwekeza katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na katika sekta za kilimo, Teknolojia ya habari na Mawasiliano na Mafuta na Gesi.

  “Ziara hii yenye wakurugenzi 30 wa kampuni mbalimbali wanataka kushirikiana na Tanzania katika sekta za Usafiri ukiwemo wa anga na ardhini,TEHAMA,Kilimo ni miongoni mwa mengine” alisema Clavier.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Uchumi na Biashara wa Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania Beatrice Alperte amesema ukuaji wa teknolojia unakwenda sambamba na ukuaji wa uchumi kwa kuzingatia tafiti ndio maana wameamua kushirikiana na Tanzania katika kukuza uwezo wa watendaji.

Biashara kati ya Tanzania na Ufaransa imekua kwa wastani wa Dola za kimarekani milioni 30 ambapo Wafanyabiashara hao wanatarajia kukutana na Rais wa Tanzania Dkk.John Pombe Magufuli,Mawaziri katika sekta mbalimbali pamoja na viongozi wa sekta binafsi TPSF nchini.

Ripoti ya Mwandishi wa Rfi Kiswahili Steven Mumbi

 

 

 

 

 

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana