Pata taarifa kuu
MALAYSIA-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa wabunge kufanyika Mei 9 nchini Malaysia

Tume ya Uchaguzi nchini Malaysia imetangaza leo Jumanne Aprili 10 kwamba uchaguzi wa wabunge utafanyika Mei 9 nchini humo. Tangazo hili linakuja siku baada ya bunge kuvunjwa na Waziri Mkuu Najib Razak.

Waziri Mkuu wa Malaysia akilihutubia taifa kuhusu kuvunjwa kwa bunge, Malaysia April 6, 2018.
Waziri Mkuu wa Malaysia akilihutubia taifa kuhusu kuvunjwa kwa bunge, Malaysia April 6, 2018. REUTERS/Lai Seng Sin TPX IMAGES OF THE DAY
Matangazo ya kibiashara

Bunge la Malaysia lilikumbwa na kashfa mbalimbali na kukabiliwa na maandamano ya raia kufuatia kupanda kwa hali ya maisha.

Waziri Mkuu Najib Razak, mwenye umri wa miaka 64, anatarajiwa kusalia madarakani, lakini wanataalam wa masuala ya kisiasa wanasema huenda uchaguzi huo ukawa na ushindani mkali, kwani waziri mkuu wa zamani Mahathir Mohamad, 92, anajaribu kufanya kila aliwezalo ili arejee kwenye wadhifa huo.

Bw Mohamed aliongoza nchi hiyo kwa mkono wa chuma kutoka mwaka 1981 hadi mwaka 2003, na kubadilisha Malaysia kurudi nyuma kimaendelea.

Mahathiri Mohamed, kama atachaguliwa, atakuwa waziri mkuu wa kwanza madarakani mwenye umri ulio mkubwa zaidi duniani.

Najib anakabiliwa na kesi kuhusu usimamizi mbaya unaohusiana na mfuko wa umma "1Malaysia Development Berhad (1MDB), ambapo dola milioni 681 ziliwekwa katika akaunti yake kibinafsi.

Najib Razak ameendelea kukanusha kuwa alifanya ubadhirifu katika kesi ya 1MDB, lakini kashfa hii ilisababisha mgawanyiko mkubwa kati yake na waziri mkuu wa zamani Mahathir, ambaye amekuwa mkosoaji wake mkubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.