Pata taarifa kuu
LIBYA-HAKI

Saadi Gaddafi afutiwa kesi ya mauaji

Mahakama ya Tripoli imefuta kesi ya mauaji iliyokua ikimkabili Saadi Gaddafi, mtoto wa tatu wa aliyekua rais wa Libya, Muammar Gaddafi.

Saadi Kadhafi (kulia) mwana wa Muammar Gaddafi, hapa akiwa kizimbani wakati kesi yake iliposikilizwa Tripoli, Machi 13, 2016.
Saadi Kadhafi (kulia) mwana wa Muammar Gaddafi, hapa akiwa kizimbani wakati kesi yake iliposikilizwa Tripoli, Machi 13, 2016. MAHMUD TURKIA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Saadi Kaddafi amefutiwa mashtaka yote dhidi yake katika kesi ya mwanamichezo Bachir al-Rayani ambaye alifariki dunia mnamo mwaka 2006 baada ya kupigwa kichwani. Bachir Rayani alifariki dunia baada ya malumbano katika nyumba inayomilikiwa na Saadi Gaddafi.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, mahakama imerejelea hukumu za maafisa wa zamani wa Libya baada ya kuhamishwa kutoka gereza la al-Hadaba kwenda sehemu iliyo chini ya usimamizi wa Wizara ya Sheria. Saadi Gaddafi alisafirishwa kutoka Niger mnamo mwaka 2014, baada ya kukimbia nchi ya Libya mnamo mwaka 2011.

Mahakama hii imemuhukumu Saadi Gaddafi kifungo cha mwaka mmoja, kwa kosa la ulevi wakati wa kifo cha rafiki yake, Bachir al-Rayani, kilichotokea katika nyumba ya Saadi Gaddafi. Mahakama ya kaskazini ya Tripoli iliahirisha hukumu yake mara kadhaa, na hatimaye ilimsafisha katika kesi ya mwanamichezo huyo.

Familia ya Bachir al-Rayani, imepinga uamuzi huo na kuelezea masikitiko yake: "Tuna ushahidi wa Saadi Gaddafi kuhusika katika kifo cha baba yetu," amesema mwanaye Bachar al-Rayani, huku akibaini kwamba watakata rufaa.

Katika ukurasa wake wa Facebook, familia ya Bachir ala-Rayani imeandika: "Ni uovu wa serikali ya zamani unaoendelea".

Kwa mujibu wa waangalizi kadhaa, uamuzi huu unaonekana kuwa ni utabiri wa kukabiliana na kesi nyingine za wakuu wa serikali ya zamani ya Libya, ambao wamekuwa wakisubiri haki kwa miaka kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.