Pata taarifa kuu

Mvutano waibuka kati ya DRC na Umoja wa Mataifa

Serikali ya DRC, pamoja na uwezo wake, inatarajia kukusanya fedha za kusaidia waathirika wa migogoro nchini humo na kutatua mgogoro wa kibinadamu unaoendelea

Wafanyakazi wa UNHCR katika Kituo cha Mapokezi cha Mussungue kaskazini magharibi mwa Angola wakitoa chakula kwa wakimbizi wa DRC waliokimbia machafuko katika mkoa wa Kasai.
Wafanyakazi wa UNHCR katika Kituo cha Mapokezi cha Mussungue kaskazini magharibi mwa Angola wakitoa chakula kwa wakimbizi wa DRC waliokimbia machafuko katika mkoa wa Kasai. Photo HCR/Adronico Marcos Lucamba
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya DRC imetangaza kwamba haitashiriki katika mkutano wa wafadhili utakaofanyika tarehe 13 Aprili Geneva, kwa jitihada za Umoja wa Mataifa.

Mkutano huu unalenga kuwezesha jumuiya ya kimataifa kupata dola bilioni 1.6 kutatua mgogoro wa kibinadamu nchini DRC.

Lakini serikali ya Kinshasa inaona kuwa ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika yasio ya kiserikali kuhusu hali mbaya ya kibinadamu nchini humo ni ya uongo.

Serikali ya DR Congo imeahidi kukusanya dola milioni 100 katika miezi 18 ijayo kusaidia waathirika wa migogoro nchini.

Mgogoro huo haujafikia ngazi iliyodaiwa na Umoja wa Mataifa, kwa mujibu wa Leonard She Okitundu, Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC. "Hali mbaya ya kibinadamu katika mikoa mitatu husika haijafikia kiwango hatari kinachodaiwa na Umoja wa Mataifa," waziri wa mambo ya nje wa DRC amesema.

"Mpango wa dharura"

Umoja wa Mataifa unaona kwamba mikoa mitatu nchini DRC imefikia kiwango cha juu cha dharura ya kibinadamu, kwenye hatua moja na Syria au Yemen, hoja ambayo waziri wa mambo ya nje wa DRC anafutilia mbali.

"Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inafahamu kabisa majukumu yake ya kukabiliana na suala hili la kibinadamu, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itazindua kwa haraka mfuko wake wa kibinadamu na mpango wake wa dharura," ameongeza Leonard She Okitundu.

Kwa mujibu wa serikali ya Kongo, takriban watu 230,000 ndio wamelazimika kuyahama makazi yao na kukimbilia maeneo salama.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, watu milioni 13 - mmoja kati ya sita nchini DRC - wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.