Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Watu 15 wauawa katika shambulio la Boko Haram Nigeria

media Vikosi vya usalama vikipiga kambi karibu na eneo la shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na Boko Harampembezoni mwa mji wa Maiduguri, Nigeria Aprili 2, 2018. REUTERS/Ahmed Kingimi

Shambulio linalodaiwa kutekelezwa na kundi la Boko Haram liliwaua watu wasiopungua15 na kuwajeruhi 68 jana Jumapili jioni katika mji wa Maiduguri kaskazini mashariki mwa Nigeria, Idara ya huduma za dharura imesema leo Jumatatu.

Washambuliaji, ambao waliopenya na kuingia katika maeneo ya Bille Shuwa na Alikaranti, maeneo mawili yalio pembezoni mwa mji karibu na kijiji cha Biwa, walirudishwa nyuma, vyanzo vya kijeshi vimesema. Milipuko kadhaa iliripotiwa wakati wa urushianaji risasi kati ya wapiganaji hao na maafisa wa usalama.

"Watu sitini na nane walijeruhiwa na watu 15 wasio na hatia waliuawa," amesema Bello Dambatta, Mkuu wa Idara ya huduma za dharura (Sema). Idadi ta vifo inaweza kuongezaka, kulingana na vyanzo vya kijeshi.

Serikali ya Nigeria ilitangaza wiki iliyopita kuwa mazungumzo na kundi la Boko Haram yalianza kwa lengo la kusitisha mapigano.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana