Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-UPINZANI

Felix Tshisekedi kupeperusha bendera ya UDPS katika uchaguzi ujao DRC

Chama cha upinzani nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya congo UDPS kimemtangaza Felix Tshisekedi kuwa mgombea wake katika uchaguzi mkuu wa raisi mnamo decemba 23 mwaka huu

FelixTshisekedi kiongozi wa UDPS nchini DRC
FelixTshisekedi kiongozi wa UDPS nchini DRC ERIC LALMAND / Belga / AFP
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza jijini Kinshasa katika ofisi za chama hicho msemaji wa UDPS Peter Kazadi amefahamisha kuwa UDPS imeamua kuweka mapambano yake vizuri kwa kumkabidhi jukumu hilo Felix Tshisekedi Tshilombo kuwania nafasi ya uraisi wa jamuhuri ya kidemokrasia ya congo.

Mkutano mkuu wa chama hicho pia ulimpitisha Tshisekedi kuwa mwenyekiti wa chama cha UDPS kwa kura 790 kati ya 803 ambayo ni asilimia 98 ya kura zote.

Kwa upande wake Felix Tshisekedi ambaye sasa anamrithi baba yake Etienne Tshisekedi , aliyefariki dunia tarehe mosi mwezi wa pili mwaka jana,baada ya kutangazwa amesema hatimaye atafanikisha ndoto za waliokuwa waasisi ikiwa uchaguzi utafanyika baadae mwaka huu.

Uchaguzi uliokuwa ufanyike mwaka 2017 mwishoni ulisogezwa mbele na sasa unatarajiwa December 23, 2018 ili kumpata mrithi wa Joseph Kabila, ambaye muhula wake wa uongozi ulitamatika December 20, 2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.