Pata taarifa kuu
SIERRA LEONE-UCHAGUZI

Sierra Leone: Wananchi kupiga kura kwenye duru ya pili Jumamosi

Wananchi wa Sierra Leone watapiga kura Jumamosi ya wiki hii katika uchaguzi wa duru ya pili, uchaguzi ambao umechelewa kwa siku nne baada ya mahakama kuusogeza mbele, wakati huu kinyang'anyiro kikitarajiwa kuwa kati ya rais wa sasa na kinara wa upinzani ambaye aliibuka na ushindi kwenye duru ya kwanza. 

Wanajeshi wakitoa ulinzi mjini Freetown kuelekea uchaguzi wa duru ya pili siku ya Jumamosi, 26.03.2018
Wanajeshi wakitoa ulinzi mjini Freetown kuelekea uchaguzi wa duru ya pili siku ya Jumamosi, 26.03.2018 REUTERS/Olivia Acland
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya raia milioni 3 na laki 1 wanatarajiwa kupiga kura kuchagua mrithi wa rais bai Koroma ambaye kwa mujibu wa katiba haruhusiwa kuwania tena baada ya kumaliza mihula yake miwili.

Matokeo ya awali yatatarajiwa kuanza kutolewa kuanzia wiki ijayo.

Katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa Machi 7, huku asilimia 84 ya wapiga kura wakijitokeza, Samura Kamara anayeungwa mkono na Koroma kupitia chama tawala ambacho kiko madarakani, apipata asilimia 41.7 ya kura.

Kinara wa upinzani kupitia muungano wa SLPP Juliuz Maada Bio aliibuka mshindi kwa asilimia 43.3 ya kura zote lakini hata hivyo asingeweza kuwa raia kwa kuwa hakufikisha asilimia 55.

Uchaguzi wa duru ya pili baina ya vyama hivi viwili ambavyo vimekuwa vikichuana tangu nchi hiyo ipate uhuru kutoka kwa mkoloni wake nchi ya Uingereza 1961m ulikuwa umepangwa kufanyika Machi 27.

Lakini wakati kampeni ambazo zilishuhudia vurugu kati ya wafuasi wa vyama hivyo viwili na kuibua hofu ya kuokea machafuko ya kikabila na zikiwa zimefikia tamati, uchaguzi ukasogezwa mbele Machi 24 baada ya rufaa iliyowasilishwa na chama tawala.

Licha ya rufaa hiyo kutupwa Jumatatu ya wiki hii na kuchelewesha uchaguzi huo, tume ya uchaguzi NEC ilitoa muda wa siku nne mbele kufanyika kwa uchaguzi huo.

Mgombea wa upinzani Bio aliongeza shinikizo kwa rais Koroma akimtuhumu kupanga njama za kuitumbukiza nchi hiyo kwenye machafuko kwa mbinu za kutaka kuchelewesha uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.