Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

UN yaipa MONUSCO mamlaka kusimamia uchaguzi DRC

media Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura. UN Photo/Loey Felipe

Baraza la usalama la umoja wa mataifa Jumanne ya wiki hii limeipa mamlaka makubwa tume yake ya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kushiriki kwenye maandalizi ya uchaguzi unaolenga kumaliza muhula wa rais Joseph Kabila.

Baraza la usalama kwa kauli moja limeridhia azimio lililowasilishwa na Ufaransa iliyotaka kuongezewa muda kwa tume ya MONUSCO nchini DRC kwa muda wa mwaka mmoja hadi Machi mwaka 2019, ikisisitiza kuwalinda raia wakati huu nchi hiyo ikijiandaa na uchaguzi mkuu mwezi Desemba.

Nchi za magharibi zimeongeza shinikizo kwa rais Kabila kuruhusu mabadilishano ya amani ya madaraka baada ya uchaguzi wa Desemba 23 na kumtaka vyombo vyake vya usalama kutoa ulinzi kwa raia baada ya kuuawa kwa waandamanaji.

Nchi ya Urusi imeonya walinda amani hao kutochukua upande wowote wakati wa uchaguz wakati balozi wa DRC kwenye umoja huo akisema tume hiyo inapaswa kujikita katika kuyadhibiti makundi ya waasi na sio kusimamia uchaguzi.

Balozi wa Ufaransa Francois Delattre amesema kura hiyo ilikuwa muhimu kwa mustakanali wa DRCna eneo la ukanda, kura aliyosema inatengeneza njia ya ubadilishanaji wa madaraka kwa amani.

"Bila kuwa na uchaguzi wa kuaminika na uliokubaliawa na watu wote, usalama wa nchi na eneo zima la ukanda litakuwa hatarini," alisema balozi huyo.

Utawala wa Kinshasa tayari umetangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu, lakini rais Kabila ambaye yuko madarakani tangu mwaka 2001 hajatangaza hadharani ikiwa ataondoka madarakani au la hatua inayozusha hofu kuwa nchi hiyo huenda ikatumbukia kwenye machafuko.

Baraza hilo limemuomba katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres kuandaa mpango wa kuongeza nguvu zaidi kwa walinda amani ikiwa itahitajika pamoja na kuongeza wanajeshi zaidi.

Guterres atatakiwa kuto ripoti kwa baraza hilo katika siku 90.

Chini ya azimio hili MONUSCO itatoa msaada wa kiufundi na usafiri wakati wa uchaguzi. kusaidia kutoa mafunzo kwa polisi na kutazama haki za binadamu na kutakiwa kuripoti kwenye baraza hilo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana