Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Zimbabwe: Rais Mnangagwa awaachia huru wafungwa 3000

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ambaye alichukua madaraka hayo toka kwa mtangulizi wake Robert Mugabe mwezo Novemba mwaka jana, amewaachia huru wafungwa zaidi ya 3000 kwa lengo la kupunguza idadi ya wafungwa ambao wamefurika kwenye magereza ya nchi hiyo.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Msamaha huu wa rais utashuhudia kuachiwa kwa wafungwa wote wa kikem walemavu na watoto huku waliohukumiwa kifungo cha maisha jela msamaha huu ukiwa hauwahusu.

Wafungwa wanaoumwa na wale ambao wamezidi umri wa miaka 60 na ambao wametumikia robo tatu ya kifungo chao pia wataachiwa huru.

“Rais kwa kufuata katiba ya Zimbabwe ametoa msamaha kwa wafungwa,” imesema taarifa ya idara ya magereza nchini humo.

Taarifa hiyo imesema kuwa jumla ya wafungwa 3000 wataachiwa huru na kufanya idadi ya wafungwa waliobakia kufikia elfu 17.

Imeongeza kuwa wafungwa ambao wanasubiri kunyongwa na ambao wameshatumikia kifungo cha miaka 10 jela hawatanyongwa tena na badala yake watatumikia kifungo cha maisha jela.

Nchi hiyo ilitekeleza adhabu ya kunyonga mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2005 na rais Mnangagwa ni mmoja wa watu walio mstari wa mbele kupinga adhabu ya kifo.

Wafungwa waliohukumiwa kwa mauaji, uhaini, ubakaji, uporaji wa magari, uporaji wa mabavu na wale waliohukumiwa na mahakama ya kijeshi hawakuhusishwa kwenye msamaha huu.

Nchi ya Zimbabwe imewaachia maelfu ya wafungwa hivi karibuni chini ya utawala wa Robert Mugabe.

Serikali inakabiliwa na ukata mkubwa wa fedha unaoifanya ishindwe kuwahudumia kwa chakula na nguo pamoja na matibabu maelfu ya wafungwa ambapo mwaka 2013 jumla ya wafungwa 100 walipoteza maisha wakiwa gerezani.

Mwaka 2015 wafungwa wanne walipoteza maisha baada ya kufanya mgomo kupinga hali mbaya za maisha gerezani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.