Pata taarifa kuu
DRC

DRC: Kayonga atupwa jela, Serikali yaanza mazungumzo kuhusu sheria ya madini

Aliyekuwa mkuu wa taasisi ya kupambana na rushwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amehukumiwa kifungo cha maisha jela na mahakama ya kijeshi baada ya kupatikana na hatua ya makosa ya uasi na mauaji mashariki mwa nchi hiyo.

Mfano wa picha ya uchimbaji madini ambayo Abbas Kayonga alikatazwa kufanya hivyo akiwa mkuu wa tume ya kupamba na rushwa nchini DRC
Mfano wa picha ya uchimbaji madini ambayo Abbas Kayonga alikatazwa kufanya hivyo akiwa mkuu wa tume ya kupamba na rushwa nchini DRC Tom Stoddart/Getty
Matangazo ya kibiashara

Abbas Kayonga alikamatwa na walinda amani wa umoja wa Mataifa mashariki mwa nchi hiyo kwenye mji wa Bukavu tarehe 5 ya mwezi Novemba mwaka jana ikiwa ni siku chache tangu afutwe kazi kwa uzembe kazini.

Juhudi za vikosi vya Serikali kujaribu kumkamata zilizusha makabiliano makali na walinzi wake ambapo watu sita walipoteza maisha kabla ya walinda amani wa umoja wa Mataifa kuingilia kati.

Alifikishwa mahakamani siku moja baadae akiwa sambamba na watu wengine 30 walioshtakiwa kwa makosa ya kufanya uasi.

Katika hukumu iliyotolewa Jumanne ya wiki hii, mahakama ilimuhukumu yeye na wengine 13 walihukumiwa kunyongwa, huku mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo akitaka wapelekwe jijini Kinshasa na kutupilia mbaloi uwezekano wa kukata rufaa.

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo adhafu ya kifungo cha maisha haitekelezwi tena na badala yake kwa makosa kama hayo mtu hutumikia kifungo cha maisha.

Watu wengine 13 walihukumiwa kifungo cha kati ya miaka 5 hadi 20 jela.

"Mahakama iliwakuta na hatia ya uasi, mauaji na kumiliki silaha kinyume cha sheria zikiwemo za kivita," alisema hakimu Riger Wavara.

Kayonga muasi wa zamani aliongoza uchunguzi wa makosa ya rushwa jimboni Kivu Kusini jimbo ambalo ni maarufu kwa madini ya dhahabu, tin na Coltan.

Hata hivyo alifutwa kazi na gavana wa jimbo hilo Novemba 2.

Katika hatua nyingine Serikali ya Kinshasa imesema tayari imeanza mazungumzo na wamiliki wa makampuni yanayochimba madini mashariki mwa nchi hiyo siku chache tu baada ya rais Joseph Kabila kutia saini sheria mpya ya madini iliyopingwa vikali na makampuni hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.