Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

UN yataka MONUSCO kupewa nguvu kuhakikisha uchaguzi huru DRC

media Wanajeshi wa kulinda amani nchini DRC walio chini ya tume ya MONUSCO. AFP/Eduardo Soteras

Baraza la usalama la umoja wa Mataifa linafikiria kupitisha pendekezo la nchi ya Ufaransa linalotaka walinda amani wa umoja huo walioko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wasaidie kuandaa uchaguzi mkuu wa kuaminika nchini humo.

Pendekezo hilo ambalo limeonwa na shirika la habari la Ufaransa AFP, linataka kuongezwa muda wa mwaka mmoja kwa tume ya MONUSCO kusalia nchini DRC na kuanisha vipaumbele wakati huu nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi wa Desemba 23.

Uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo utatoa njia ya kubadilishana madaraka kutoka kwa rais Joseph Kabila ambaye alichukua hatamu ya uongozi toka kwa marehemu baba yake Mzee Desire Kabila aliyeuawa mwaka 2001.

Tume ya uchaguzi nchini DRC tayari imetangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo lakini rais Joseph Kabila bado hajatangaza hadharani ikiwa atawania tena au la, hali inayoibusha hofu kuwa huenda nchi hiyo ikatumbukia kwenye machafuko.

Pendekezo la nchi ya Ufaransa limesisitiza kuhusu umoja wa Mataifa kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa uchaguzi wa Desemba 23, 2018 unaandaliwa katika mazingira ya uwazi, kuaminika, shirikishi pamoja na usalama.

Ufaransa inataka tume ya MONUSCO kupewa jukumu la kuwalinda raia na kusaidia mchakato wa uchaguz ikiwemo usajili wa wapiga kura, kura yenyewe na makabidhiano ya madaraka Januari 12 mwakani.

Hatua zilizopendekezwa na Ufaransa pia zinamtaka katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Antonio Guterres kutengeneza mpango wa kuongeza nguvu zaidi kwa walinda amani wake ikiwa itahitajika.

Katibu mkuu Guterres atatakiwa kuripoti kwa baraza la usalama baada ya siku 90 tangu azimio hilo kupitishwa akieleza kwa kina mpango wa kuhakikisha uchaguzi huru na haki nchini DRC.

Baraza la usalama linatarajiwa kupigia kura azimio hilo Machi 27 mwaka huu, na wanadiplomasia wanasema kuwa wanatarajia azimio hilo kupitishwa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana