Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Nigeria: Boko Haram yawaachia huru wasichana wengine wa Dapchi

media Wasichana wa shule ya ufundi kwenye eneo la Dapchi wakiwa wanamsubiri rais Muhammadu Buhari kuwasili hivi karibuniarch 14, 2018. REUTERS/Ola Lanre

Kundi la kiislamu la Boko Haram nchini Nigeria ambalo liliwateka nyara wasichana 110 wa shule kwenye mji wa Dapchi kaskazini mwa nchi hiyo mwezi mmoja uliopita mpaka sasa limewaachia wasichana 101 wa shule, Serikali imesema.

Waziri wa habari Lai Mohammed amesema wasichana hao waliachiwa bila masharti au kubadilishana fedha.

Waziri Mohammed ameongeza kuwa "kwa sasa idadi ya wasichana wanaofahamika kuachiwa na kundi hili ni 101."

Fatima Gremah mwenye umri wa miaka 13 ambaye ni mmoja wa walioachiwa, amewaambia wanahabari kuwa viongozi wa kundi hilo waliwaambia wana bahati kwakuwa ni wadogo na ni waislamu.

"Mmoja wetu ambaye alikuwa mkristo amebakishwa, wamesema wataendelea kumshikilia hadi pale atakapobadili dini," alisema msichana huyo.

"Ikiwa ataslimu watamuachia. Ni yeye peke yake kati yetu ndiye aliyesalia."

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alisema juma lililopita kuwa Serikali yake imeamua kutumia njia ya majadiliano  ili kuhakikisha wasichana hao wanaachiwa bila masharti badala ya kutumia jeshi.

Mohammed amesema kuwa kuachiwa huru kwa wasichana wa Dapchi kumtokena na juhudi za marafiki wa nchi hiyo ambao hata hivyo hakutaja majina yao waliofaniksha zoezi la kuachiwa kwao.

Serikali imetangaza pia kusitishwa kwa operesheni zote za kijeshi kwenye mji wa Dapchi ili kuruhusu mabadilishano ya amani ya wasichana hao na kuwafanya wasipoteze maisha bila sababu.

Tukio la wasichana kutekwa kwenye mji wa Dapchi Februari 19 kumerejesha machungu ya tukio jingine la utekwaji wa wasichana wa shule kwenye eneo la Chibok mwezi April mwaka 2014 ambapo wasichana zaidi ya 200 walitekwa.

Aisha Alhaji Deri mwenye umri wa miaka 16 ambaye alikuwa miongoni mwa waliotekwa kwenye eneo la Dapchi, amewaambia wanahabari kuwa hawakunyanyaswa walipokuwa wakishikiliwa.

Lakini akaongeza kuwa watano kati yao walipoteza maisha wakati walipkuwa wakichukuliwa.

"Waliturudisha asubuhi na kutushusha kwenye gereji na kutuambia twende nyumbani na sio kwa wanajeshi ambao watadai wametuokoa."

Wasichana hai wamedai kuwa kwa muda wote walikuwa wakishikiliwa kwenye kisiwa cha ziwa Chad, eneo ambalo linafahamika kuwa ngome kubwa ya wapiganaji wa Boko Haram na kiongozi wa enei hilo Abu Mus'ab al-Barnaw.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana