Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Kenya: Faru wa mwisho mweupe aliyekuwa amebaki duniani amekufa

media Faru mweupe wa kike Najin na mwanae, faru wawili wa mwisho wa kike waliobakia wakiwa kwenye hifadhi ya Ol Pejet nchini Kenya. REUTERS/Baz Ratner

Faru dume wa mwisho mweupe amekufa nchini Kenya akiwa na umri wa miaka 45 huku akiwaacha faru wawili wakike pekee walio hao na wa jamii yake, wamesema waliokuwa wakiwatazama faru hao.

Faru huyo aliyepewa jina la Sudan, "alikuwa akitibiwa kwa muda mrefu tatizo la misuli na mifupa lililosababisha vidonda visivyopona," imesema taarifa ya shirika la Ol Pejeta lililokuwa linatoa ulinzi kwa faru huyo.

Faru Sudan ndiye faru pekee mweupe aliyekuwa amebaki hai duniani na alikuwa akipatiwa hifadhi chini ya ulinzi mkali nchini Kenya.

"Hali yake ilizorota vibaya katika saa 24 zilizopita; alikuwa hawezi tena kusimama na alionesha maumivu makali, wamesema madaktari waliokuwa wakimtifu faru huyo kabla ya kufanya uamuzi wa kumchoma sindano kusitisha uhai wake."

Madaktari hao wamesema kuwa kifo cha faru Sudan kinahitimisha rasmoi kinadharia kuwa, faru wa aina hii ndio wametoweka rasmi duniani.

Hata hivyo wanasayansi wamefanikiwa kupata vinasaba kutoka kwa faru huyo na wanaendelea na vipimo vya maabara kupata njia ya kuvifanya vijizalishe ili kulinda farua hao adimu duniani.

Fru weupe wa kaskazini waliokuwa wakipatikana nchini Uganda, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan na Chadi walipotea kwa kiwango kikubwa wakati wa wimbi la uwindaji haramu kwenue miaka ya 1970 na 1980, hali iliyotokana na mahitjai makubwa ya pembe za faru kwaajili ya tiba za asili nchini China na Yemen.

Faru pekee waliobakia kati ya 20 na 30 waliokuwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliuawa kutokana na mapigano kwenye miaka ya 90 na 200 na kufikia mwaka 2008 ilitangazwa kuwa faru hao walikuwa wametoweka kabisa.

Faru wa nne wenye uwezo wa kuzaa, wawili wa kike na wawili wa kiume walihamishwa kutoka hifadhi ya Dvur Kralove, Jamhuri ya Czech na kupelekwa kwenye hifhadhi ya Ol Pejeta nchini Kenya kukiwa na matumaini kuwa huenda wakiishi kwenye mazingira waliyozoea watawashawishi kuzaana.

Hata hivyo licha ya kuonekana kuwa walikuwa wakijamiiaana hapakuwa na mafanikio ya faru wa kike kupata ujauzito.

Jaribio la kuchukua vinasaba vya faru dume na kuviweka kwa faru jike navyo havikufua dafu.

Faru mwingine wa kiume aliyepewa jina la Suni alifariki mwaka 2014 kwa sababu za kawaida.

"Sudan alikuwa faru mweupe wa mwisho kuzaliwa msituni na kifo chake ni pigo kutokana na uharibifu uliofanywa na binadamu," amesema Jan Stejskal mkurugenzi wa mradi wa kimataifa kwenye hifadhi ya Dvur Kralove.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana