Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika
DRC

Francophone: DRC yawa mstari wa mbele katika matumizi ya lugha ya Kifaransa

media Waziri wa habari na msemaji wa Serikali ya DRC, Lambert Mende akizungumza hivi karibuni, Alhamisi ya wiki hii amekosoa kauli ya Ufaransa Reuters

Wakati nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa zikiadhimisha siku ya kimataifa ya lugha hiyo, maarufu kama la Francophonie, Nchi ya DRC imeonekana kuipa lugha hiyo kipao mbele miongoni mwa mataifa mengine ya jumuia ya nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa.

Mfano ulio hai ni katika soko kubwa la jiji kuu la Kinshasa Grand Marche ambako watoza ushuru wanaitumia lugha hiyo ya kifaransa wakati wanapotoza ushuru kwa wafanyabiashara ambao asilimia kubwa wanawasiliana kwa Kutumia lugha ya Lingala.

Ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na wataalamu wa kitaifa kuhusu masuala ya utamaduni imebainisha kuwa kwa sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ina wakaazi kati ya milioni sabini hadi 90 na ndio nchi kubwa inayozungumza Kifaransa duniani, ikifuatiwa na Ufaransa yenye wakaazi kama milioni 67.

Katiba ya nchi ya DRC imeainisha kuwa kifaransa ndio lugha kuu, inayowaunganisha wananchi kwenye taifa hilo, ikifuatiwa na lugha nyingine nne za kitaifa kama vile Lingala inayozungumzwa mjini Kinshasa na maeneo mengine ya magharibi, Kiswahili katika sehemu kubwa ya mashariki mwa taifa hilo, Tshiluba katika majimbo ya Kasai ya katikati mwa taifa hilo na Lugha ya Kikongo huko Matadi.

Akinukuliwa na gazeti la Ufaransa la Le Figaro, mtafiti Henri Leridon amesema asilimia hamsini ya wananchi huko DRC wanazungumza lugha ya kifaransa, na kwamba asilimia ndogo ndio wanaoongea lugha ya Lingala na Kiswahili,huku Kiswahili ikiwa ni lugha inayozungumzwa Kusini mwa Jangwa la Sahara na nchi za Afrika mashariki ikiwa ni pamoja na Kenya, Uganda, na Tanzania.

Katika kuikuza lugha hiyo, serikali ya ufaransa kupitia ubalozi wake nchini DRC ilizinduliwa taasisi ya lugha ya kifaransa katika mji wa Goma jirani na Rwanda, mashariki mwa nchi hiyo, mwezi oktoba mwaka jana.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana