Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Zimbabwe: Rais Mnangagwa ataja majina ya watu na makampuni yaliyoficha fedha nje

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amechapisha mamia ya majina ya watu na makampuni ambayo yameshindwa kurejesha kiasi cha dola za Marekani milioni 827 ambazo wamezihifhadhi nje ya nchi hiyo kinyume cha sheria.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa. REUTERS/Philimon Bulaway
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuchukua madaraka kama rais mwaka uliopita, rais Mnangagwa alitoa muda wa siku 90 kwa watu na makampuni kurejesha kiasi hicho cha fedha kwa kubadilishana na msamaha.

Rais Mnangagwa amesema agizo lake limesababisha kurejeshwa kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 591 ikiwa ni chini ya nusu ya kiasi kinachodhaniwa kuwa kimefichwa nje ya nchi hiyo.

Kiongozi huyo kwenye taarifa yake aliyoitoa juma hili amesema wale walioshindwa kurejesha ndani ya muda aliokuwa ameutoa watakabiliwa na mkono wa sheria.

Wakati akiingia madarakani rais Mnangagwa aliapa kupambana na vitendo vya rushwa ambapo amesema uvumilivu umemhsinda na kuamua kutangaza majina 1800 yanayojumuisha viwanda, madini, biashara ndogondogo, makanisa na hata mashirika ya uma.

Majina haya yamegawanywa katika makundi matatu ambapo wamo waliopeleka fedha zao kwenye akaunti za nje, makampuni yaliyoagiza vitu na fedha hizo kutoingia nchini humo na raia wa kawaida wanaodaiwa kuficha fedha zao kwenye mabenki ya nje.

Makampuni ya uchimbaji madini ndio yanayoongoza kwenye orodha hiyo ambapo kiujumla yanatakiwa kurejesha kiasi cha dola za Marekani 150.

Katika hatua nyingine rais Mnangagwa ametangaza kuwa nchi yake itafanya uchaguzi mkuu wake wa kwanza wa rais na wabunge mwezi Julai mwaka, ikiwa ni uchaguzi wa awali tangu kuondoka madarakani kwa Robert Mugabe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.