Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 10/12 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 10/12 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 09/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Mahakama ya China yazuia mauzo ya iPhone kufuatia ombi la Qualcomm
 • Nadia Murad, mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel 2018, aomba "ulinzi wa kimataifa" kwa jamii ya Yazidi
 • Nchi itayoandaa michuano ya AFCON 2018 itajulikana Januari 9 kwa mujibu wa rais wa Shirikisho la Soka Afrika
Afrika

Rwanda: Nigeria kutotia saini mkataba wa biashara huria kwa bara la Afrika

media Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari. REUTERS/Dan Kitwood

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari hatahudhuria kikao cha wakuu wa nchi za umoja wa Afrika AU kinachofanyika jijini Kigali, Rwanda juma hili, hatua ambayo imekuwa pigo katika mpango wa kuzindua na kutia saini mkataba wa biashara huruia kwenye nchi wanachama 54 ya umoja huo.

Mkutano wa juma hili jijini Kigali ulilenga kuzindua rasmi mkataba wa biashara huria kwa bara la Afrika, mkataba ambao baraza la mawaziri la Nigeria liliuridhia Jumatano ya wiki iliyopita.

Rais Buhari alitarajiwa kuondoka mjini Abuja Jumatatu ya wiki hii kuhudhuria sherehe za siku ya Jumatano, lakini akajiondoa kwa kile alichodai nchi yake inahitaji majadiliano zaidi kabla ya kuutia saini.

Taarifa ya ikulu ya Nigeria imesema kuwa "Rais hatasafiri tena kwenda Kigali kwaajili ya shughuli hiyo kwa kuwa baadhi ya wadau nchini mwake wamedai kuwa hawakushirikishwa na kwamba wanayomasuala yanayowagusa kwenye mkataba huo," imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa "Uamuzi wa rais Buhari ni kwa lengo la kutoa muda zaidi wa kufanyika kwa majadiliano ya kina kuhusu mktaba huo."

Miongoni mwa wadai waliomtaka rais Buhari kutotia saini mkataba huo ni pamoja na shirikisho la wafanyakazi.

Taasisi mbalimbali za wafanyakazi nchini humo zimedai kuwa mkataba huo utaenda kupigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la uchumi wa nchi hiyo ambao tayari unayumba.

Umoja wa Afrika uliamua kuendelea mbele na mkataba huu mwaka 2012 uliolenga kuanzishwa kwa soko la pamoja kwaajili ya ubadilushanaji wa bidhaa na huduma.

Mkataba huu unatengeneza majadiliano ya kimfumo ili kupanua biashara za ndani kuanzia kwenye ngazi ya chini kabisa kwa asilimia 14, imesema taarifa ya rais Buhari.

Nchi ya Nigeria ambayo ni mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika ina jumla ya idadi ya watu milioni 190 na ina soko kubwa.

Jumla ya wakuu wa nchi 26 wanatarajiwa kuhudhiria shughuli za utiaji saini mkataba huu jijini Kigali.

Umoja wa Afrika unasema soko la pamoja lipo kwenye agenda ya mwaka 2063, kuhusu muungano wa baraa la Afrika, ambapo Afrika itakua na sauti moja katika kuimarisha biashara kati ya bara hilo na mabara mengine.

Takwimu zinaonesha kuwa biashara kati ya nchi za afrika ni asilimia 16%.

Mkataba huu ambao utahusisha nchi wanachama 54 zenye idadi ya watu zaidi ya bilioni 1 utasaidia kuongeza biashara ya ndani ya bara hilo kwa zaidi ya asilimia 14 iliyopo kwa sasa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana