Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Mshindi wa urais nchini Sierra Leone kuamuliwa kupitia duru ya pili

media Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Sierra Leone Mohamed Nfa'ali Conteh,akitanagza matokeo ya mwisho ya urais Machi 13 2018 jijini Freetown www.voanews.com

Wananchi wa Sierra Leone sasa watalazimika kwenda kwenye duru ya pili ya uchaguzi tarehe 27 mwezi Machi mwaka huu baada ya mgombea wa chama kikuu cha upinzani kupata ushindi ambao haukumuwezesha kumshinda mgombea wa chama tawala katika duru ya kwanza ya uchaguzi.

Kinara wa upinzani Julius Maada Bio kutoka chama cha Sierra Leone People SLPP alitangazwa mshindi kwa kupata asilimia 43.3 ya kura katika uchaguzi wa Machi 7 wakati mgombea wa chama tawala cha All People's Congress Samura Kamara akipata asilimia 42.7 ya kura.

Wawili hao watapambana katika duru ya pili na mshindi, kuunda serikali.

Tume ya uchaguzi imesema, matokeo haya yameonesha karibu asilimia 85 ya watu walishiriki kwenye uchaguzi huu ambao ulishuhudia wapiga kura milioni 3.1 wakijiandikisha.

Kwa mujibu wa sheria za uchaguzi nchini humo mshindi wa jumla alitakiwa kupata asilimia 55, uchaguzi ambao umeshuhudiwa vyama hivi viwili vikiongoza taifa hilo tangu uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1961.

Waangalizi wa uchaguzi kutoka ndani na nje ya nchi wameendelea kutoa ripoti zao za awali ambapo wamesema uchaguzi ulikuwa huru, haki na wakuaminika licha ya vurugu zilizoripotiwa kwenye miji ya Freetown na kaskazini mwa Kono.

Mgombea wa chama cha tatu Kande Yumkella alimaliza kwa kupata asilimia 6.9 licha ya matumaini ambayo muungano wake wa kitaifa ulitarajiwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana