Pata taarifa kuu
TANZANIA-UFARANSA-FRANCOPHONIE

Mabalozi wahimiza amani na Utulivu katika nchi za Francophonie

Mabalozi wa nchi 10 za Jumuiya ya Kimataifa ya nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa, Francophonie wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wamesema muungano wao unahamasisha kufuatwa kwa utawala wa sheria pasipo kuingilia uhuru wa nchi mwanachama.

Mabalozi kutoka nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa Francophonie wakiongozwa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frédéric Clavier (Katikati) wakizindua wiki ya kuhimiza lugha ya Kifaransa nchini Tanzania Machi 14 2018
Mabalozi kutoka nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa Francophonie wakiongozwa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frédéric Clavier (Katikati) wakizindua wiki ya kuhimiza lugha ya Kifaransa nchini Tanzania Machi 14 2018 RFI/Emmanuel Makundi
Matangazo ya kibiashara

Akizungumzia jijini Dar es salaam,Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier amesema migogoro ya kisiasa inayojitokeza katika nchi mwanachama imekuwa ikitatuliwa kupitia jukwaa maalumu la viongozi.

“Jumuiya yetu inahamasisha amani usalama na utulivu wa nchi na kuheshimu haki za binadamu lakini pia tunaheshimu tamaduni na uhuru wa nchi kwa hiyo ni uchaguzi wa wakuu wa nchi kuhakikisha maendeleo na utawala bora unafikiwa” alisema Clavier

Balozi Clavier ametoa kauli hiyo baada ya RFI Kiswahili kutaka kujua muungano huo una wajibu gani katika kuhamasisha utawala wa sheria na ukuaji wa demokrasia katika nchi wanachama barani Afrika kama vile DRC na Burundi.

Mabalozi kutoka nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa nchini Tanzania walipokutana jijini Dar es salaam, kuzindua wiki ya francophonie, Machi 14 2018
Mabalozi kutoka nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa nchini Tanzania walipokutana jijini Dar es salaam, kuzindua wiki ya francophonie, Machi 14 2018 RFI Kiswahili/Emmanuel Makundi

Aidha wakati dunia ikiadhimisha miaka 17 ya azimio la kimataifa la haki za binadamu, muungano huo unazitaka nchi wanachama kuendelea kuheshimu haki za binadamu na utawala ambapo balozi wa Uswisi nchini Tanzania Florence Mattli anasema jijini Dar es salaam watakuwa wanaonyesha tukio hilo litakalofanyika katika nchi yake.

“Siku hiyo tutaungana na dunia katika kuonyesha umuhimu wa kuheshimu haki za binadamu kama ilivyo Francophonie inahamasisha kuheshimu haki hizo na tutaonyesha kinachofanyika Uswis katika umoja huo” alisema Mattli.

Katika maadhimisho haya ya wiki moja shughuli mbalimbali zitakuwa zikiendelea kwa juma zima ikiwemo michezi, maonesho ya filamu zilizorekodiwa kwa lugha ya kifaransa, maigizo yanayoonesha uhusiano wa kitamaduni kutoka Canada.

Susan Steffen ni Balozi wa msaidizi wa Canada nchini Tanzania anasema wataonyesha filamu fupi inayoonesha mashirikiano ya kiutamaduni baina ya nchi zenye tamaduni tofauti.

Lugha ya Kifaransa inazungumzwa na karibu watu milioni 200 duniani na inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2050 watu zaidi ya milioni 700 watakuwa wanazungumza Kifaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.